• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 26, 2014

  MISRI WATWAA UBINGWA WA U17 AFRIKA KASKAZINI

  Na Salum Esry, Rabat
  MISRI imetwaa ubingwa wa soka wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa nchi za Kaskazini mwa Afrika (UNAF) baada ya kuwafunga wenyeji Morocco mabao 3-1 katika fainali Uwanja wa Prince Moulay El Hassan Sports Complex mjini Rabat.
  Mafarao Wadogo wameibuka mabingwa wa mashindano hayo yaliyoanza Machi 21 na kufikia tamati Machi 23, 2014.
  Misri ilipata bao la kwanza dakika ya 18 kupitia kwa Hossam Adel kabla ya Mohamed Hamdy kufunga la pili dakika ya 35.
  Misri iliifunga Morocco 3-1 mjini Rabat na kutwaa Kombe
  Zouhair Idriss aliifungia bao moja Morocco sekunde chache kabla ya mapumziko, lakini Mohamed Alaa akafunga la tatu dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho.

  Katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Tunisia waliwafunga Libya 2-0 na kujinyakulia Medali ya Shaba.
  Timu nne zilishiriki mashindano hayo ya siku nne yaliyoandaliwa na Umoja wa Vyama vya Soka Kaskazini mwa Afrika (UNAF) na ni Algeria pekee ambayo haikushiriki kati ya nchi wanachama wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MISRI WATWAA UBINGWA WA U17 AFRIKA KASKAZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top