• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 28, 2014

  NATURE, PROFESA JAY NA JAY MOE WATOA WIMBO KWA PAMOJA UITWAO JWTZ, WATUMIA ZANA HALISI ZA JESHI KATIKA VIDEO YAO

  Na Dina Ismail, Dar es Salaam
  WASANII watatu wakongwe na maarufu wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’, Juma Kassim ‘Nature’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’ wamerekodi kwa pamoja wimbo uitwao JWTZ.
  Wimbo huo umerekodiwa kwa sauti na video katika studio za Williamz Visions chini ya mtayarishaji Mike Mwakatundu ‘Mike T’.
  Profesa Jay akiimba katika moja ya maonyesho Dar es Salaam

  Mike T maarufu kama Mnyalu, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, yeye anakuwa muongozaji wa kwanza wa video au filamu Tanzania kupata fursa ya kutumia vifaru, ndege, helikopta na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika kazi zake.
  “Naamini kwa kumtanguliza Mungu kila kitu kinawezekana, baada ya yote, naamini magwiji hao wamefanya kweli,”amesema Mike T, ambaye pia ni gwiji wa Bongo Fleva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NATURE, PROFESA JAY NA JAY MOE WATOA WIMBO KWA PAMOJA UITWAO JWTZ, WATUMIA ZANA HALISI ZA JESHI KATIKA VIDEO YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top