• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 21, 2014

  MAN UNITED NA BAYERN, BARCA NA MADRID ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA

  KLABU ya Manchester United itakutana na mabingwa watetezi, Bayern Munich katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya droo iliyomalizika kupangwa muda huu mjini Nyon, Uswisi.
  Timu nyingine pekee ya England iliyobaki katika michuano hiyo, Chelsea imepelekwa kwa mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain baada ya kuchaguliwa na Luis Figo.
  Mechi nyingine ni kati ya timu za Hispania tupu Barcelona na Atletico Madrid wakati Real Madrid itamenyana na Borussia Dortmund ya Ujerumani.

  Mwali: Taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya likiwa mjini Nyon, Uswisi wakati wa upangaji wa droo ya Robo Fainali

  ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA 2014

  Barcelona vs Atletico Madrid
  Real Madrid vs Borussia Dortmund
  Paris Saint-Germain vs Chelsea
  Manchester United vs Bayern Munich
  Mechi za kwanza zitachezwa Aprili 1 na 2, wakati marudiano itakuwa Aprili 8 na 9.
  In the mix: Wayne Rooney and Manchester United are outsiders for the competition after scraping through
  Mtihani mgumu: Wayne Rooney na Manchester United watatapambana na mabingwa watetezi, Bayern Munich
  Happy? Samuel Eto'o and Chelsea eased past Galatasaray in the round of 16 after a 2-0 win at Stamford Bridge
  Furaha? Samuel Eto'o na Chelsea waliitoa Galatasaray Hatua ya 16 Bora
  Big boys: Real Madrid's Cristiano Ronaldo (right) and Gareth Bale are looking to deliver another trophy
  Majina makubwa: Wachezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (kulia) na Gareth Bale kushoto
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED NA BAYERN, BARCA NA MADRID ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top