• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 31, 2014

  ISHA MASHAUZI AIBUKA NA KITU SURA SIYO ROHO

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam 
  MWANAMUZIKI na kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ametoa nyimbo mpya mbili, ambazo muda si mrefu zitaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya Redio nchini.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii katika hoteli ya Double Tree, Masaki, Dar es Salaam wakati wa semina ya wanamuziki waliongia kwenye tuzo za Kili 2014, Isha au Jike la Simba amesema kwamba nyimbo zote ni nzuri.
  'Jike la Simba' Isha Mashauzi ana nyimbo mpya mbili

  Amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Sura Siyo Roho na Mapenzi Hayana Dhamana ambazo zote ametunga yeye mwenyewe.
  “Kama kawaida, wapenzi na mashabiki wangu na mashabiki wa Mashauzi Classic kwa ujumla, wajiandae kwa kazi mpya, tutaanza na audio (sauti) baadaye itafuatia na kwenye video pia,”alisema Isha. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ISHA MASHAUZI AIBUKA NA KITU SURA SIYO ROHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top