• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 29, 2014

  CHELSEA YAPIGWA KIDUDE NA CRYSTAL PALACE, UBINGWA SASA...

  KLABU ya Chelsea imeangukia pua katika mbio za ubingwwa Ligi Kuu ya England baada ya kufungwa bao 1-0 na Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park.
  Chelsea inayofundishwa na kocha Mreno Jose Mourinho, liingia wikiendi hii ikiwa inaongoza mbio za ubingwa dhidi ya wapinzani wake, Manchester City na Liverpool na rekodi ya kutofungwa na timu za London.
  The Blues iliifunga Arsenal 6-0 wikiendi iliyopita, lakini kwa wapinzani wao wa 10 wa London bao la kujifunga la beki John Terry dakika ya limeipa Palace ushindi wa 1-0 huo ukiwa ushindi wao wa kwanza katika ligi dhidi ya Chelsea kwa takriban miaka 24.
  Huo ni mchezo wa pili mfululizo The Blues wanafungwa ugenini, baada ya awali kufungwa na Aston Villa na sasa inabaki na pointi zake 69 za mechi 32 mbele ya Liverpool yenye 68 za moja 31.
  Masikitiko: Mchezaji wa Crystal Palace, Jason Puncheon (kushoto) akishangilia huku Terry akisigina kichwa chake chini baada ya kujifungaOwn goal: Chelsea captain John Terry heads the ball over goalkeeper Petr Cech to put into his own net
  La kujifunga: Nahodha wa Chelsea, John Terry akipiga kichwa kutumbukiza mpira kwenye lango la kipa wake, Petr CechAll smiles: Crystal Palace players celebrate Terry's own goal as supporters go wild in the stands
  Wachezaji wa Crystal Palace wakishangilia ushindi wao
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAPIGWA KIDUDE NA CRYSTAL PALACE, UBINGWA SASA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top