• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 30, 2014

  LIVERPOOL 'MABOSI' LIGI KUU ENGLAND, WAIFUMUA 4-0 SPURS NA KUREJEA KILELENI

  KLABU ya Liverpool imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya Tottenham Uwanja wa Anfield jioni hii.
  Kaboul alianza kujifunga dakika ya pili kuipatia Liverpool bao la kwanza kabla ya Luis Suarez kufunga la pili dakika ya 25, Coutinho la tatu dakika ya 55 na Henderson la nne dakika ya 76.
  Kwa ushindi huo mnono, Liverpool sasa inatimiza pointi 71 baada ya kucheza mechi 32 na kupaa kileleni ikiishusha Chelsea yenye pointi 69 za mechi  32 pia, wakati Manchester City yenye pointi 67 za mechi 30 ni ya tatu na Arsenal yenye pointi 64 za mechi 32 ni ya nne.
  Kileleni: Liverpool imepaa kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya kuifumua 4-0 Tottenham Hotspur
  Menace: Suarez was a constant threat to the Spurs defenders
  Mtaalamu huyo: Suarez akimpiga chenga beki wa Spurs
  No touch: Suarez tries to get a touch on Henderson's free-kick
  Mpiganaji: Suarez akipambana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL 'MABOSI' LIGI KUU ENGLAND, WAIFUMUA 4-0 SPURS NA KUREJEA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top