• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 21, 2014

  ARSENAL WAMKABIDHI TUZO YA DHAHABU LEO WENGER KUTIMIZA MECHI 1,000

  KOCHA Arsene Wenger leo amekabidhiwa tuzo ya dhahabu kwa kufikisha mechi 1,000 akiwa kazini Arsenal.
  Mfaransa huyo atafikisha mechi ya 1,000 kesho atakaposafiri na The Gunners hadi Stamford Bridge kumenyana na Chelsea katika Ligi Kuu ya England mchana.
  Kuheshimu hilo, Mwenyekiti wa Arsenal, Sir Chips Keswick amemkabidhi Wenger tuzo hiyo leo asubuhi katika viwanja vya mazoezi ya klabu mbele ya Waandishi wa Habari.
  Washika Bunduki: Wenger akiwa na Mtendaji Mkuu, Ivan Gazidis (kushoto) na Mwenyekiti Sir Chips Keswick (kulia) baada ya kupokea tuzo yake

  Akizingatia wa timu kufanya vizuri na kufanya vibaya akiwa kazini, Wenger aliyeipa timu hiyo mataji matatu ya Ligi Kuu ya England na manne ya Kombe la FA, alisema; "Kila kipigo unachopata ni maumivu moyoni ambayo huwezi kusahau, na kila ushindi ni wa kusahau kwa sababu unachukuliwa ni kawaida,".
  Aliongeza; "Kumekuwa na msoto mkubwa katika mechi 1,000. Kitu ninachotaka wakati ujao wa furaha,"alisema.
  New arrival: Wenger was an unknown when he turned up at Highbury in September 1996
  Alipowasili: Wenger alikuwa hafahamiki wakati anatambulishwa Uwanja wa Highbury (sasa Emirates) Septemba mwaka 1996
  Double trouble: Wenger hoists the Premier League trophy while captain Tony Adams lifts the FA Cup after Arsenal won the Double in 1997-1998
  Wakati wa furaha: Wenger akiwa ameshika taji la ubingwa wa Ligi Kuu wakati Nahodha, Tony Adams akiwa ameshika Kombe la FA baada ya Arsenal kushinda mataji mawili msimu wa 1997-1998
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL WAMKABIDHI TUZO YA DHAHABU LEO WENGER KUTIMIZA MECHI 1,000 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top