• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 25, 2014

  RAIS FA YA LIBERIA ATETEA NAFASI YAKE

  Na Prince Akbar, Dar es Salaam
  RAIS wa Chama cha Soka Liberia, Hassan Musah Bility amefanikiwa kutetea nafasi yake hiyo katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi nchini humo.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliyotumwa BIN ZUBEIRY leo, imesema Bility, ambaye amekuwa akishikilia wadhifa huo tangu Machi mwaka 2010 ametetea nafasi yake hiyo katika uchaguzi uliofanyika mji wa tatu kwa kubwa wa nchi hiyo Magharibi mwa Afrika, Buchanan na kuhudhuriwa na Wajumbe 51 kati ya 54.
  Anaendelea kula bata; Hassan Musah Bility amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Liberia

  Katika uchaguzi huo, Musa H. Shannon alichaguliwa tena kuendelea kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Cassell A. Kuoh Makamu wa Pili na Ciata Bishop – Female alichagauliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.
  Wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Ansu Dulleh, Wallace G. Weiah, Samuel Y. Karn, Sheba Brown, Rochell G.D. Woodson, John Allan Klayee, Matthew P. Smith, Dee-Maxwell Kemeyah na Urias Glaybo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa CAF, Almamy Kabele Camara alikuwepo kwenye uchaguzi huo pamoja na Ofisa Maendeleo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa nchi za Afrika Magharibi, Sampon Kablan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAIS FA YA LIBERIA ATETEA NAFASI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top