• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 31, 2014

  ZAMALEK YAIFUMUA 5-0 NKANA, YATINGA NANE BORA LIGI YA MABINGWA...MWAKA HUU KAZI IPO HIZO TIMU ZILIZOFUZU

  Na Salum Esry, Cairo
  KLABU ya Zamalek ya Misri imefanikiwa kutinga Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya jana kuifunga Nkana FC ya Zambia mabao 5-0 Uwanja wa Jeshi la Anga mjini Cairo. 
  Sasa timu hiyo ya kocha Ahmed Hassan ‘Mido’ imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-0 baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza mjini Kitwe wiki iliyopita.
  Jana Ahmed Tawfik alifunga bao la kwanza dakika ya 20 kabla ya Momen Zakrya kufunga la pili na Zamalek walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza 2-0. 
  Wachezaji wa Zamalek wakishangilia ushindi wao jana

  Kipindi cha pili Omar Gaber akafunga la tatu, Hazem Emam la nne na Ahmed Gafer la tano.
  Zamalek sasa imeungana na Al Ahli Benghazi ya Libya, TP Mazembe ya DRC, CS Sfaxien ya Tunisia,
  Vita Club ya Kongo, Esperance ya Tunisia, El Hilal ya Sudan na Entente Setif ya Algeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZAMALEK YAIFUMUA 5-0 NKANA, YATINGA NANE BORA LIGI YA MABINGWA...MWAKA HUU KAZI IPO HIZO TIMU ZILIZOFUZU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top