// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIIZA KATIKA WAKATI MGUMU YANGA SC, AAMBIWA HATA PENALTI ALIIKIMBILIA TU, LAKINI ALIYETAKIWA KUPIGA NI CANNAVARO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIIZA KATIKA WAKATI MGUMU YANGA SC, AAMBIWA HATA PENALTI ALIIKIMBILIA TU, LAKINI ALIYETAKIWA KUPIGA NI CANNAVARO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 20, 2014

    KIIZA KATIKA WAKATI MGUMU YANGA SC, AAMBIWA HATA PENALTI ALIIKIMBILIA TU, LAKINI ALIYETAKIWA KUPIGA NI CANNAVARO

    Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
    HAMISI Friday Kiiza jana alitoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo analia baada ya kutolewa ‘maneno machafu’ na wapambe wa viongozi wa Yanga SC kwa kukosa penalti jana timu hiyo ikitoka sare ya 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Chumba cha kubadilishia nguo cha Yanga SC jana kiligeuka kama eneo la shimoni sokoni Kariakoo kwa kelele na matusi baada ya mchezo huo, wapambe wa viongozi wakiwatukana wachezaji kwa kushindwa kuifunga Azam jana.
    Majuto mjukuu; Hamisi Kiiza alibaki yeye na kipa,lakini Aishi Manula akabki
    Kipa Aishi Manula aklipangua penalti ya Kiiza 

    Ni Kiiza aliyekuwa katika wakati mgumu zaidi, akilaumiwa kwamba mbali na kukosa penalti, pia alipata nafasi nyingi akashindwa kuzitumia. 
    Walidai hata penalti aliikimbilia tu, wakati mtu aliyetakiwa kwenda kupiga alikuwa Nahodha ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
    Wapambe hao pia walimlaumu kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kwa kutomuanzisha Mrisho Ngassa ambaye jana aliingia dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Didier Kavumbangu. 
    Azam ilicheza kwa zaidi ya dakika 20 za mwisho ikiwa pungufu jana baada ya beki wake wa kulia, Erasto Nyoni kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kutoa lugha chafu kwa refa, Hashim Abdallah.
    Yanga SC walitangulia kupata bao lililofungwa na mshambuliaji kutoka Burundi, Didier Kavumbangu dakika ya 14 aliyekutana na mpira uliorudi baada ya kupanguliwa na kipa Aishi Salum Manula kufuatia kutokea piga nikupige langoni mwa Azam. 
    Shambulizi lililozaa bao hilo lilianzia kwa kwa Simon Msuva aliyemtoka beki Gadiel Michael wingi ya kulia na kutia krosi iliyounganishwa na Kavumbangu lakini mpira ukagonga mwamba na kurudi uwanjani na kumkuta Hamisi Kiiza aliyepiga kipa akaokoa na kumkuta mfungaji aliyemaliza kazi.
    Yanga SC ilipata penalti dakika ya 69 kufuatia beki Said Mourad ‘Mweda’ kuunawa mpira uliopigwa na Didier Kavumbangu, hata hivyo mkwaju wa Hamisi Kiiza ‘Diego’ ulipanguliwa vizuri na kipa Aishi Salum Manula na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda. 
    Baada ya kona hiyo wachezaji wa Azam wa Azam FC walikwenda kumlalamikia refa ambaye alimuonyesha kadi ya pili ya njano Erasto Nyoni na kuwa nyekundu.
    Pamoja na kubaki wachache, Azam waliendelea na jitihada za kusaka bao la kusawazisha na dakika ya 83 kinda aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili, Kevin Friday aliipokea vyema pasi ya Salum Abubakr ‘Sure Boy’ na kumchambua kipa mkongwe Juma Kaseja.
    Azam FC sasa inajiongezea pointi moja na kufikisha pointi 44 baada ya mechi 20, wakati Yanga SC inatimiza pointi 40 baada ya mechi 19.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIIZA KATIKA WAKATI MGUMU YANGA SC, AAMBIWA HATA PENALTI ALIIKIMBILIA TU, LAKINI ALIYETAKIWA KUPIGA NI CANNAVARO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top