• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 25, 2014

  RAIS WA AL AHLY ILIYOITOA YANGA AKAMATWA NA KUSWEKWA RUMANDE KWA RUSHWA

  Na Tarek Talaat, Cairo
  RAIS wa Al Ahly ya Misri, ambayo iliitoa Yanga SC ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi huu, Hassan Hamdi amekamatwa na kuwekwa gerezani akikabiliwa na kesi nzito ya rushwa.
  Hamdi alikamatwa Jumapili na atabaki huko kwa siku 15 ili asiweze kutoroka Misri hadi uchunguzi utakapokamilika. Hamdy amekanusha tuhuma zote dhidi yake.
  Rushwa zako hazikuingia Yanga?
  Rais wa Al Ahly, Hassan Hamdi
  anakabiliwa na kesi nzito ya rushwa

  Hassan Mahmoud Hamdi Ismail aliyezaliwa mwaka 1949 ni Rais wa 13 wa vigogo hao wa Misri, Al Ahly na pia ni Mwenyekiti wa kampuni ya Al-Ahram Advertising Agency, ambayo ni sehemu ya Al-Ahram Association .
  Hamdi ambaye aliichezea Al Ahly katika nafasi ya ulinzi kuanzia 1969 hadi 1978, alikuwa Rais wa klabu hiyo mwaka 2002 baada ya Rais wa zamani, Saleh Salim kufariki dunia. BIN ZUBEIRY itaendelea kufuatilia maendeleo ya kesi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAIS WA AL AHLY ILIYOITOA YANGA AKAMATWA NA KUSWEKWA RUMANDE KWA RUSHWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top