• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 29, 2014

  MAN UNITED WAITANDIKA 4-1 ASTON VILLA, ROONEY APIGA MBILI

  FURAHA imerudi katika nafsi ya kocha David Moyes kufuatia Manchester United kuifunga mabao 4-1 Aston Villa Uwanja wa Old Trafford jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. 
  Mabao mawili yaliyofungwa na Wayne Rooney dakika za 20 na 45 kwa penalti na mengine ya Juan Mata dakika ya 57 na Javier Hernandez dakika ya 90 yalitosha kuiongezea pointi United.
  Villa ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ashley Westwood dakika ya 13 kwa mpira wa adhabu.
  United sasa inatimiza pointi54 baada ya kucheza mechi 32 na inaendelea kubaki nafasi ya saba nyuma ya Tottenham Hotspur yenye pointi 56 za mechi 31.

  Babu kubwa: Wayne Rooney amefunga mabao mawili leo Manchester United ikiifunga Aston Villa 4-1Inside out: As Mata turns inside Bacuna the defender takes the Spanish midfielders legs out
  Juan Mata akipambana na Bacuna 
  Cool and calm: Rooney powered the penalty into the side netting with precision leaving Guzan no chance
  Rooney akifunga kwa penalti
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED WAITANDIKA 4-1 ASTON VILLA, ROONEY APIGA MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top