• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 23, 2014

  MESSI AVUNJA MLANGO UWANJA WA TAIFA BAADA YA KIPIGO CHA COASTAL, POLISI WAMGWAYA, ASINDIKIZWA NA BAUNSA

  Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
  KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ anadaiwa kuvunja kioo cha mlango wa chumba cha kubadilishia nguo cha timu yake leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mechi dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Wakundu wa Msimbazi wakifungwa 1-0.
  Pamoja na ushahidi uliotolewa na wafanyakazi wa Uwanja wa Taifa kwa askari Polisi kwamba, Messi ndiye aliyevunja kioo, hicho lakini wachezaji wenzake na viongozi wa Simba SC walimtetea.
  Amevunja mlango? Ramadhani SIngano 'Messi' anadaiwa kuvunja mlango (pichani chini) Uwanja wa Taifa leo

  Polisi walishindwa kuchukua hatua yoyote kuhofia kusababisha vurugu na mchezaji huyo aliondoka uwanjani hapo kuelekea kwenye basi la timu yake akisindikizwa na baunsa. 
  Tukio hilo limechukuliwa kama hasira za kipigo cha bao 1-0 nyumbani mbele ya Coastal Union katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AVUNJA MLANGO UWANJA WA TAIFA BAADA YA KIPIGO CHA COASTAL, POLISI WAMGWAYA, ASINDIKIZWA NA BAUNSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top