• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 31, 2014

  MWANA FA ANA NYIMBO TATU MPYA, LAKINI HAJUI ATOE IPI

  Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam 
  HAMISI Mwinjuma au Mwana FA ana nyimbo tatu mpya zilizokamilika, lakini hajui aanze kuitambulisha ipi.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo wakati wa semina ya wanamuziki walioingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Kili 2014, FA amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Mfalme, Kiboko Yangu na Tandale Au Masaki.
  Wimbo Mfalme (Wooii) umerekodiwa na prodyuza Nahreel ambaye hurekodi nyimbo za Weusi na amemshirikisha G Nako, wakati Kiboko Yangu umerekodiwa na Marco Chali na amemshirikisha Ally Kiba.
  Mwana FA ana nyimbo tatu, lakini hajui atambulishe ipi kwanza

  FA amesema kwamba wimbo Tandale Au Masaki kila kitu kipo tayari, lakini bado haujarekodiwa tu na amepanga wiki ijayo aingie studio.
  “Hizi nyimbo zote ni kali, ndiyo maana zinanichaganya, sijui niutambulishe upi kwanza, ila muda si mrefu nitapata jibu,”alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MWANA FA ANA NYIMBO TATU MPYA, LAKINI HAJUI ATOE IPI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top