// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA YAZIDI KUUDOGELEA UBINGWA ENGLAND, YAIFUMUA FULHAM 3-1 YOTE APIGA SCHURRLE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA YAZIDI KUUDOGELEA UBINGWA ENGLAND, YAIFUMUA FULHAM 3-1 YOTE APIGA SCHURRLE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 01, 2014

    CHELSEA YAZIDI KUUDOGELEA UBINGWA ENGLAND, YAIFUMUA FULHAM 3-1 YOTE APIGA SCHURRLE

    KIUNGO Mjerumani, Andre Schurrle amefunga mabao matatu peke yake kipindi cha pili na kuiwezesha Chelsea kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham jioni hii.
    Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alitarajia safari ya katikati ya wiki Istanbul katika Ligi ya Mabingwa ingewachosha wachezaji wake na kucheza kichovu Craven Cottage, lakini licha ya mwanzo mgumu ilipata mabao matatu ndani ya dakika 16 na kuendelea kuwa kileleni mbele ya Arsenal na Manchester City kwenye mbio za ubingwa.
    Schurrle alifunga mabao hayo dakika za 52, 65 na 69, wakati bao la kufutia machozi la Fulham lilifungwa na Heitinga dakika ya 74 na Chelsea sasa inatimiza pointi 63 baada ya kucheza mechi 28, ikifuatiwa na Arsenal pointi 59 mechi 28 na Manchester City pointi 57 mechi 26 wakati Liverpool ni ya nne pointi 57 mechi 28.
    Shujaa wa Hat-trick: Andre Schurrle akishangilia baada ya kukamilisha mabao matatu ndani ya dakika 16 peke yake
    Best man: Schurrle celebrates after turning in his third goal
    Mchezaji bora: Schurrle akishangilia baada ya kufunga bao la tatu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YAZIDI KUUDOGELEA UBINGWA ENGLAND, YAIFUMUA FULHAM 3-1 YOTE APIGA SCHURRLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top