• HABARI MPYA

    Saturday, March 01, 2014

    ARSENAL YALAMBWA KIDUDE NA STOKE, UBINGWA SASA LABDA!

    MATUMAINI ya Arsenal kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England yamezidi kufifia baada ya jioni hii kuchapwa 1-0 na Stoke City, bao pekee la Jon Walters kwa penalti kipindi cha pili.
    Walters alikwenda kuukwamisha nyavuni mkwaju huo dakika ya 76 baada ya Laurent Koscielny wa Arsenal kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
    Matokeo hayo na ushindi wa Chelsea dhidi ya Fulham, inamaanisha Arsenal walio nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, sasa wanazidiwa pointi nne na The Blues huku zikiwa zimebaki mechi 10 kukamilisha msimu.
    Wakati huo huo, Manchester City walio nafasi ya tatu wanazidiwa pointi mbili na Arsenal na wana mechi mbili mkononi.
    Furaha: Jonathan Walters akishangilia na Peter Crouch baada ya kufunga penalti iliyoipa Stoke ushindi wa 1-0From 12 yards: Walters sent Szczesny the wrong way from the spot to open the scoring
    Miguu 12 ya mtu mzima: Walters akimpoteza maboya kipa wa Arsenal Szczesny Down: Arsenal look dejected as they fall four points behind Chelsea at the top of the Premier League
    Hoi: Wachezaji wa Arsenal baada ya kufungwa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YALAMBWA KIDUDE NA STOKE, UBINGWA SASA LABDA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top