• HABARI MPYA

    Thursday, November 14, 2013

    YONDAN AWAPA ‘GWALA’ MADOGO STARS, ILA AWAONYA…

    Na Mahmoud Zubeiry, Ilala
    MCHEZAJI bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kevin Patrick Yondan amesifu uwezo wa wachezaji wa timu ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars na amesema wakiendelea hivyo watalisaidia taifa lao na kupata mafanikio binafsi.
    Akizungumza jana baada ya mechi baina ya timu ya kwanza ya taifa, Taifa Stars na Future Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam jana, beki huyo wa Yanga alisema kwamba vijana walicheza vizuri na anaamini wote ni wachezaji wazuri
    “Wanatakiwa wajitambue wao ni hazina ya taifa, hata sisi tumetokea kule, hivyo waongeze bidii, wasije kulewa sifa wakaishia njiani,”alisema Yondan, beki tegemeo wa kati wa Taifa Stars.
    Wanaweza, ila wasilewe sifa; Kevin Yondan amewapongeza wachezaji wa Future Young Taifa Stars 

    Yondan alisema anaamini baada ya mechi ile, kocha wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen atakuwa amepata wachezaji 10 wa kuongeza Taifa Stars kutoka Future kama alivyodhamiria kwa kuwa vijana walionyesha uwezo wa jana.
    Future Young Taifa Stars jana ilionyesha ina wachezaji wengi wazuri, baada ya kuifunga Taifa Stars 1-0, bao pekee la mshambuliaji wa Ruvu Shooting ya Pwani, Elias Maguri aliyeunganisha krosi ya chipukizi wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Juma Luizio.
    Kabla ya kutia krosi, Luizio alimpokonya mpira beki mkongwe wa Yanga na mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Kevin Yondan ambaye alianzishiwa na kipa wake, Ally Mustafa ‘Barthez’.
    Kwa ujumla Future waliihenyesha Stars inayoundwa na wachezaji nyota wa Tanzania wakiwemo Mrisho Ngassa, ambaye hii leo alishindwa kufurukuta.
    Kikosi cha Furure kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’ (Yanga)/Aishi Manula (Azam), Michael Pius (Ruvu Shooting)/John Kabanda (Mbeya City)/Kessy Hamisi (Mtibwa Sugar), Himid Mao (Azam FC)/Hassan Mwasapili (Mbeya City), Ismail Gamba ‘Kussi’ (Azam Akademi), Said Mourad (Azam FC), Jonas Mkude (Simba), Ramadhani Singano ‘Messi’ (Simba SC)/Joseph Kimwaga (Azam FC), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Elias Maguri (Ruvu Shooting)/Paul Nonga (Mbeya City), Juma Luizio (Mtibwa Sugar)/Farid Mussa (Azam FC) na Haroun Chanongo/(Simba B)Simon Msuva/(Yanga SC) na Hussein Javu (Yanga SC). 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YONDAN AWAPA ‘GWALA’ MADOGO STARS, ILA AWAONYA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top