DROO YA NUSU FAINALI
Bayern Munich v Barcelona
Borussia Dortmund v Real Madrid
Bayern itamenyana na Barcelona Aprili 23 na Mei 1, wakati Dortmund na Real zitakutana April 24 na 30.
*Timu zilizopangwa kushoto katika ratiba zitacheza mechi ya kwanza nyumbani
SOMA RATIBA KAMILI YA NUSU FAINALI HAPA
KUNA nafasi ya mechi ya Clasico kupigwa Wembley kwa ajili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na Real Madrid na Barcelona kutenganishwa katika mechi za Nusu Fainali za michuano hiyo.
Jose Mourinho na kikosi chake cha Real kimepangwa na Borussia Dortmund, wakati Barcelona itamenyana na Bayern Munich, maana yake ni viya ya Waspanyola na Wajerumani kuwania safari ya Wembley Mei 25.
Dortmund ni timu pekee iliyobaki kwenye michuano hii ambayo haijapoteza mechi hadi sasa na itakutana na Real kwa mara ya pili msimu huu katika mashindano haya. Mabingwa hao wateteri wa Bundesliga, walikuwa vinara wa kundi la kifo, lililoihusisha Real, Manchester City na Ajax.
Barabarani: Jose Mourinho anaweza kuifikisha Real Madrid Wembley katika fainali ya Ligi ya Mabingwa?