• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 28, 2013

  STURRIDGE APIGA MBILI LIVERPOOL IKIIKUNG'UTA NEWCASTLE 6-0 ST JAMES PARK


  MSHAMBULIAJI Daniel Sturridge leo amevaa viatu vya Luis Suarez na kuendeleza vyema kampeni za Liverpool ikiifumua Newcastle ya kocha Alan Pardew mabao 6-0.
  Mshambuliaji huyo, ambaye alifiungia Chelsea kwenye Uwanja huo wa St James Park msimu uliopita, leo amefunga mabao mawili katika ushindi huo dakika za 50 na 64. Mabao mengine yalifungwa na Agger dakika ya tatu na Henderson dakika ya 17 na 76.
  Kikosi cha Newcastle kilikuwa: Elliot, Debuchy, Steven Taylor, Yanga-Mbiwa, Haidara, Sissoko, Tiote/Anita dk65, Cabaye,Perch/Ben Arfa dk46, Gutierrez/Gouffran dk46 na Cisse.
  Liverpool: Reina, Johnson, Carragher, Agger, Jose Enrique, Henderson, Gerrard/Borini dk72, Lucas, Coutinho/Suso dk84, Sturridge/Shelvey dk84 na Downing.

  Rout: Two-goal Daniel Sturridge takes the ball past Newcastle's Jonas Gutierrez
  Safari: Mfungaji wa mabao mawili ya Liverpool, Daniel Sturridge akimtoka mchezaji wa Newcastle, Jonas Gutierrez
  More to come: Jordan Henderson wheels away in celebration after scoring his first goal
  Mengi yanakuja: Jordan Henderson akishangilia bao lake la kwanza
  Dance: Sturridge laps up the appreciation after his goal
  Dansi: Sturridge akiserebuka baada ya kufunga 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: STURRIDGE APIGA MBILI LIVERPOOL IKIIKUNG'UTA NEWCASTLE 6-0 ST JAMES PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top