• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 20, 2013

  CAVANI KUWA MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI ENGLAND, MAN CITY YAMUANDALIA KITITA KUFURU


  KLABU ya Manchester City inajiandaa kumfanya Edinson Cavani mchezaji anayelipwa zaidi England, kwa kumpa mshahara wa Pauni Milioni 13.3 kwa mwaka.
  Lakini bado City itatakiwa kupambana na Real Madrid, katika kuwania saini ya mshambuliaji huyo, kwani hao ndio wapinzani wao wakuu kwenye vita ya kumuwania mchezaji huyo wa Napoli.
  City imeonyesha dalili za kupiga hatua fulani katika kumuwania mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay, baada ya wiki kadhaa za mazungumzo na wawakilishi wake. 
  City bound: Edinson Cavani is set to become the highest-paid player in England with a £13.3m-per-year deal close to being signed
  Anakwenda City: Edinson Cavani anajiandaa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi England kwa mshahara wa Pauni Milioni 13.3 anaokaribia kusaini

  Na inafahamika majadiliano kuhusu vipengele vya maslahi binafsi ya Cavani katika mkataba yapo karibu kumalizwa ikiwemo suala la posho na mshahara na atakuwa akiweka kwenye pochi lake Pauni 256,000 kwa wiki.
  Dau hilo litawapiku mshambuliaji mwingine wa City, Carlos Tevez na wa Manchester United, Wayne Rooney, ambao wote wanalipwa Pauni 250,000 kwa wiki.
  Cavani, pamoja na mchezaji anayetakiwa na Chelsea, Radamel Falcao, watakuwa wachezaji gumzo katika dirisha lijalo usajili.
  Mbali na maslahi yake binafsi, lakini pia klabu yake itataka Pauni Milioni 52 kumruhusu mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuondoka, ingawa City wanatarajiwa kuomba punguzo la ada ya uhamisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CAVANI KUWA MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI ENGLAND, MAN CITY YAMUANDALIA KITITA KUFURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top