• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 21, 2013

  FABREGAS AING'ARISHA BARCELONA LA LIGA, SASA UBINGWA NJE NJE


  BAO la dakika za lala salama la Cesc Fabregas, jana limeipa Barcelona ushindi wa 1-0 dhidi ya Levante siku ambayo Eric Abidal alicheza mechi yake ya kwanza tangu afanyiwe upasuaji wa ini, akicheza dakika zote 90.
  Huku mfungaji tegemeo wa timu Lionel Messi akiwa nje kwa maumivu yake ya nyama za paja la kulia ili awe fiti kabisa kabla ya kumenyana na Bayern Munich katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa, safu ya ushambuliaji ya Barcelona ilikosa makali yake mbele ya Levante hadi  Fabregas alipofunga dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho. 
  Late intervention: Cesc Fabregas celebrates the winner
  Ushindi wa jioni: Cesc Fabregas akishangilia bao lake la ushindi
  Ushindi huo unaisogeza Barcelona karibu kabisa na ubingwa wa La Liga, sasa ikiwa inaongoza kwa pointi 13 zaidi zikiwa zimebaki raundi sita. 
  David Villa alipata nafasi nzuri ya kuifungia Barcelona dakika ya 17, baada ya mchezaji wa Levante, Papakouly Diop kumchezea rafu kwenye eneo la hatari Andres Iniesta.
  Rock solid: Barcelona's Eric Abidal (right) kept Levante and Robert Acquafresca (left) in check
  Eric Abidal (kulia) akitafuta mbinu za kumdhibiti mchezaji wa Levante, Robert Acquafresca
  Lakini kipa Keylor Navas akazuia mchomo wa penalti wa Villa. Barcelona ina pointi 84 sasa, na bado inaweza kuvuna 18 zaidi ikishinda mechi zake zote zilizobaki hivyo inaweza kufikia rekodi ya Real Madrid ya pointi 100 msimu uliopita ili kupita kabisa.
  Beki mwenye umri wa miaka 33, Abidal alicheza kwa mara ya kwanza jana tangu alipoichezea timu yake ya taifa, Ufaransa mara ya mwisho  katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ujerumani  Februari 29, mwaka 2012. Mechi yake ya mwisho Barcelona alicheza siku tatu kabla.
  Abidal alicheza mechi mbili akitokea benchi Barcelona baada ya kupona tatizo la ini mwaka jana. Na hiyo ni baada ya kufanyiwa upasuaji ini Machi mwaka 2011. Anaweza kucheza zaidi haswa kutokana na sasa mabeki wa kati wa timu hiyo, Carles Puyol na Javier Mascherano wote kuwa majeruhi.
  Mkataba wa Abidal unaisha Juni mwaka huu na tayari amesema angependa kuendelea kucheza kwa msimu mmoja au miwili zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: FABREGAS AING'ARISHA BARCELONA LA LIGA, SASA UBINGWA NJE NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top