• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 25, 2013

  SERIKALI 'YAFUTA' MECHI YA SIMBA NA RUVU SHOOTING TAIFA LEO

  Simba SC

  Na Boniface Wambura
  MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
  Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.
  Ligi hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SERIKALI 'YAFUTA' MECHI YA SIMBA NA RUVU SHOOTING TAIFA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top