• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 26, 2013

  HAPATOSHI AZAM NA COASTAL MKWAKWANI, BINGWA LIGI KUU KUPATIKANA LEO?

  Mabao vipi? John Bocco 'Adebayor'
  muda mrefu hajafunga Ligi Kuu, leo vipi?


  MECHI ZILIZOBAKI ZA BIG THREE
  AZAM FC: 
  Aprili 27, 2013;  Vs Coastal Union (Chamazi)
  Mei 11, 2013;    Vs Mgambo JKT  (Chamazi)
  Mei 18, 2013;    Vs JKT Oljoro      (Arusha)

  P W D L GF GA GD Pts
  2 Azam FC 23 14 5 4 41 19 22 47

  SIMBA SC:
  Aprili 28, 2013; Vs Polisi Moro       (Taifa)
  Mei 5, 2013;      Vs Ruvu Shooting (Taifa)
  Mei 8, 2013;      Vs Mgambo JKT   (Taifa)
  Mei 18, 2013;    Vs Yanga SC        (Taifa)

  P W D L GF GA GD Pts
  4 Simba SC 22 9 9 4 32 21 11 36

  YANGA SC:
  Mei 1, 2013;    Vs Coastal Union  (Taifa)
  Mei 18, 2013;  Vs Simba SC        (Taifa)

  P W D L GF GA GD Pts
  1 Yanga SC 24 17 5 2 44 13 31 56
  Na Mahmoud Zubeiry
  BINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom anaweza kupatikana leo, iwapo Azam FC itashindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa ugenini leo dhidi ya wenyeji Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Mkwakwani.
  Inafahamika mbio za ubingwa msimu huu zimebaki kuwa za farasi wawili sasa, Yanga SC walio kileleni kwa pointi zao 56 na Azam FC wenye pointi 47, ambao wakishinda mechi zao zote tatu zilizobaki watafakisha pointi 56, ambazo tayari wapinzani wao wanazo. 
  Maana yake, matokeo mengine yoyote tofauti na ushindi dhidi ya Coastal leo, yatamaanisha Yanga imetwaa taji la 24 la ubingwa wa Ligi tangu mwaka 1968 walipotwaa mara ya kwanza na la tatu ndani ya miaka mitano.
  Azam haijakata tamaa ya kuifukuza Yanga SC na imepania kushinda leo dhidi ya Coastal ili kuona mwisho wa mbio hizi utakuwaje.
  Kikosi cha Azam kipo Tanga tangu Jumatano, ingawa kimekwenda bila nyota wawili wa kikosi cha kwanza, Joackins Atudo na Khamis Mcha ‘Vialli’ ambao ni majeruhi.
  Lakini kocha Stewart Hall hana wasiwasi ana wachezaji wa kutosha kumpa pointi tatu Mkwakwani leo, katika safu ya ulinzi akimtumia Aggrey Morris badala ya Atudo na Erasto Nyoni badala ya Waziri Salum, wakati Seif Abdallah Karihe atacheza badala ya Khamis Mcha.
  Salum Abubakar ‘Sure Boy’ hatacheza leo, kwa sababu Stewart anahofia anaweza kuumia kwenye Uwanja ‘mbovu’ na akamkosa kwenye mechi muhimu mwishoni mwa wiki ijayo dhidi ya FAR Rabat nchini Morocco.
  Kwa msimu wa pili mfululizo, Azam imemudu kuwa mshindani wa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara, jambo ambalo vigogo Simba na Yanga wameshindwa.
  Yanga walikuwa nje ya mbio za ubingwa msimu uliopita na msimu huu mabingwa watetezi na wapinzani wao wa jadi, Simba SC wapo nje.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: HAPATOSHI AZAM NA COASTAL MKWAKWANI, BINGWA LIGI KUU KUPATIKANA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top