• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 30, 2013

  BILIONEA WA MAN CITY SHEIKH MANOUR KUWEKEZA DOLA MILIONI 100 KUANZISHA TIMU MPYA MLS

  MMILIKI wa Manchester City, Sheikh Mansour wa Abu Dhabi yupo karibuni kuwekeza kiasi cha dola za Kimarekani, Milioni 100 kuanzisha timu mpya itakayoshiriki katika Ligi Kuu ya Marekani, ijulikanayo kama Major League Soccer ambayo itakuwa na maskani New York.
  Bilionea huyo wa waliokuwa mabingwa wa Ligi Kuu England, amekuwa katika mazungumzo mazito na ya siri na MLS kwa miezi kadhaa juu ya kuingiza timu mpya ya nguvu USA.
  BIN ZUBEIRY inafahamu dili hilo limekaa vizuri kufanikisha na Sheikh ana matumaini yeye na Maofisa wa MLS, watakuwa kwenye nafasi ya kutangaza mpango huo wakati kikosi cha Roberto Mancini kitakapokwenda Marekani kucheza na Chelsea Jijini New York katika mchezo maalum wa hisani mwishoni mwa mwezi ujao.
  New ambitions: Sheikh Mansour (centre) wants to start an MLS franchise... and it could cost $100m
  Malengo mapya: Sheikh Mansour (katikati) anataka kuwekeza MLS dola Milioni 100
  Treading on toes: Thierry Henry already plays for the New York Red Bulls
  Wakali zaidi wataungana naye: Thierry Henry tayari anacheza New York Red Bulls
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BILIONEA WA MAN CITY SHEIKH MANOUR KUWEKEZA DOLA MILIONI 100 KUANZISHA TIMU MPYA MLS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top