• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 28, 2013

  SIMBA SC YAWACHINJA 2-1 POLISI MOROGORO

  LICHA ya kuwafunga mabao 2-1 maafande wa Polisi Morogoro jioni hii, Simba itaendelea kushika nafasi ya nnne ya msimu mamo wa ligi kuu soka tanzania Bara.
  Aidha, maafande hao nao wamezidi kujichimbia kaburi lao la kushuka daraja kwani matokeo hayo yatawabakisha katika nafasi ya pili kutoka mwisho.
  Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini dar es salaam, Polisi ilikuwa ya kwanza kuzitikisa nyavu za Simba dakika 10 bada ya kuanza kwa mchezo kupitia kwa Bantu Admin.
  Admin alifunga bao hilo baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na hivyo kupiga shuti lililotinga kirahisi langoni mwa Simba.
  Bao hilo lilipelekea wachezaji wa Simba kuzinduka kwa kuanza kucheza kwa nguvu zote ambpo  Haruna Chanongo aliisawazishia Simba, bao ambalo lilidumu hadi dakika 45 za kwanza za mchezo huo zinamalizika.
  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kidogo ambapo dakika mbili tu baada ya kuanza Mrisho Ngasa aliwainua mashabiki wa Simba baada ya kuifungia bao la pili .
  Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 39 ikiwa nyuma ya Kagera Sugar inayoshika nafasi ya tatu kwa pointi 41, wakati Azam Fc inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 48 huku mabingwa wapya wa ligi hiyo, Yanga Sc ikiwa na pointi 56.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA SC YAWACHINJA 2-1 POLISI MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
  Scroll to Top