• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 23, 2013

  AFRICAN LYON, JKT RUVU KUUMANA CHAMAZI

  Kikosi cha JKT Ruvu

  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 24 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya wenyeji African Lyon na JKT Ruvu.
  Mechi hiyo namba 165 itachezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Kamishna Hamisi Kisiwa wa Dar es Salaam. Waamuzi wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Hashim Abdallah, Omari Kambangwa, Abdallah Selega na Said Ndege wote wa Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AFRICAN LYON, JKT RUVU KUUMANA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top