• HABARI MPYA

    Tuesday, April 23, 2013

    HIVI NDIVYO MAN UNITED ILIVYOTWAA MATAJI YOTE 20 YA LIGI KUU ENGLAND NA HAKUNA KAMA FERGUSON


    UBINGWA wa Manchester United jana umeifanya klabu hiyo iweke rekodi nyingine.
    Taji hilo linakuwa la 13 kwa Sir Alex Ferguson katika misimu 21, lakini United pia sasa inakuwa klabu yenye mafanikio zaidi katika soka ya England kihistoria kwa kutwaa mataji 20.
    Kutoka taji lao la kwanza mwaka 1908, hadi kikosi cha maajabu cha 'Busby Babes' miaka ya 1950, 'Holy Trinity' miaka ya 1960 na mafanikio ya Ferguson kwa miaka 20 iliyopita, mashabiki wa United wana mengi ya kutazama nyuma juu ya makali ya timu yao.
    Katika picha hizi maalum, BIN ZUBEIRY kwa msaada wa Sportsmail inakuletea picha moja moja kutoka kila enzi za mafanikio ya Mashetani Wekundu.

    1907-08: MANGNALL NA MEREDITH WAIWEZESHA UNITED KUTWAA TAJI LA KWANZA

    Manchester United team in 1908
    Kikosi kilichotwaa taji la kwanza mwaka 1908. Ernest Mangnall (kulia kabisa) aliiongoza United katika mafanikio hayona ni sahihi kwamba Mangnall, Sir Matt Busby na Sir Alex Ferguson tu ndio wameipa mataji United. Sandy Turnbull (aliyekaa katikati chini, wa tatu kutoka kulia) alifunga mabao 25 katika mechi 30, wakati mshambuliaji Billy Meredith (aliyekaa kushoto kabisa) alikuwa mmoja wa nyota wakubwa wa timu. United ilishinda mechi 13 kati ya 14 za mwanzo ikimaliza msimu inaizidi kwa pointi tisa Aston VIlla. Ni sahihi kufikiria huu ulikuwa mwanzo wa mafanikio ya United na sasa Mashetani hao Wekundu wana mataji 20 ndani ya miaka 105. 

    1910-11: UNITED YAWAPIKU VILLA KUTWAA TAJI LA PILI NDANI YA MISIMU MINNE 

    Manchester United 1911
    Kikosi cha Manchester United kilichotwaa taji la pili 1910-11 kikiipiku Aston Villa. Ushindi wa 4-2 dhidi ya Villa katika mchezo mkali na kuwafanya waingie katika mechi ya kuwania taji dhidi ya Sunderland, ambayo pia walishinda 5-1, huku Harold Halse (wa pili kushoto nyuma) akifunga mabao mawili.

    1951-52: BUSBY AMALIZA KIU YA MUDA MREFU YA MATAJI UNITED

    Jack Rowley playing against Preston in 1952
    Mashabiki wa United walilazimika kusubiri kwa muda mrefu tangu watwae taji la mwisho, walipomaliza kileleni. Arsenal na Tottenham wote walikuwa wapinzani wa United kwenye mbio za ubingwa msimu huo, na ushindi wa mechi mbili dhidi ya The Gunners ulimaliza kazi ngumu ya timu ya Sir Matt Busby. Ushindi wa 6-1 dhidi ya Arsenal katika siku ya mwisho ya msimu uliipa taji United. Hii ni picha ya Jack Rowley Uwanja wa Preston msimu huo - Rowley ni mmoja wa wafungaji wa kihistoria Man United, na alikuwa katika kiwango cha juu msimu huo, akifunga mabao 30 katika mechi 40 za ligi.

    1955-56: KIKOSI CHA BUSBY CHAENDELEZA FURAHA YA MATAJI

    Manchester United centre forward Tommy Taylor scores his team's third goal against Chelsea at Old Trafford in 1956. Chelsea goalkeeper Mathews and brothers John and Peter Sillett look on helplessly
    Kikosi cha makinda kilichoongozwa na Sir Matt Busby kieliendelea heshim msimu huo. United ilimaliza msimu ikiwazidi pointi 11 Blackpool na Wolves na kutwaa taji la pili miaka 1950. United ilikuwa inacheza soka maridadi ya kuvutia kwa kushambilia, na ilifahamika ulimwengu mzima kama 'Busby Babes'. Miongoni mwa nyota wa msimu huo ni Duncan Edwards na Eddie Colman, na mshambuliaji Tommy Taylor. Picha hii inamuonyesha Taylor (kushoto kabisa) akifunga bao lake la pili na la tatu kwa United katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Chelsea Uwanja wa Old Trafford. Taylor alimaliza msimu na mabao 25 katika ligi.

    1956-57: UNITED YATWAA MFULULIZO MATAJI MAKINDA YA BUSBY YAKIENDELEA KUNG'ARA TENA

    Manchester United 4 v Sunderland 0, 1957 - Billy Whelan flies into the net
    United ilitwaa mfululizo mataji 1956-57, kitu ambacho hawakufanya tena hadi mwishoni mwa miaka ya 1990. Sir Bobby Charlton akiwa kivutio katika kikosi cha Sir Matt Busby msimu huu, kikiundwa na wachezaji makinda kama Duncan Edwards na Tommy Taylor walioisaidia United kutwaa taji. Waliwazidi kwa pointi nane Tottenham na Preston. Ushindi wa 4-0 dhidi ya Sunderland Uwanja wa Old Trafford ulikamilisha mpango mzika kwa United - hii ni picha ya juhudi za Billy Whelan akifunga kwa kichwa. Mkali Whelan alifunga mabao mawili siku hiyo, huku Edwards na Taylor wakifunga mengine. Whelan, Edwards na Taylor walikuwa miongoni mwa wachezaji wa United waliofariki kwenye ajali ya ndege ya Munich Air mwaka 1958, janga ambalo lilizimisha kikosi cha makinda cha Busby.

    1964-65: UNITED YAIPIKU LEEDS KUTWAA TAJI LA KWANZA MIAKA YA SITINI

    Manchester United's Denis Law (second r) fires his team's third goal past Arsenal goalkeeper Jim Furnell (r, diving), watched by teammate David Herd (c) and Arsenal's Ian Ure (l) and Frank McLintock (second l)
    Taji la kwanza kati ya mawili ya miaka ya 1960 United lilipatikana msimu wa 1964-65, Wekundu hao wakiwapiku Leeds kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Huku winga kinda George Best akianza kujijengea jina, na Denis Law akisimama mbele ya lango la adui, United iliwapiku wapinzani wao wa Yorkshire. Ushindi wa mbinde wa 1-0 Uwanja wa Elland Road, Aprili, lililofungwa na John Connelly, uliweka mambo sawa. United ilitwaa taji baada ya kuwafunga 3-1 Arsenal Uwanja wa Old Trafford, siku ambayo Leeds ilitoka sare na Birmingham. Hii ni picha ya Law akifunga bao la pili, na la tatu kwa United dhidi ya Gunners.

    1966-67: 'HOLY TRINITY' ALIPOIWEZESHA UNITED KUTWAA TAJI TENA

    Sir Matt Busby and players celebrate league title in 1967
    Sir Matt Busby aliiongoza United kutwaa taji la pili ndani ya misimu mitatu 1966-67, Wekundu hao wakiwazidi kwa pointi nne Nottingham Forest na Tottenham. Magwiji wa klabu, 'Holy Trinity' akina George Best, Denis Law na Sir Bobby Charlton walikuwa kila kitu katika mafanikio haya na United wakawa mabingwa kwa mara ya saba. Law alifunga mabao 23 kwa United msimu huo na Mscotland huyo alifunga mabao mawili wakati United ikiitandika West Ham 6-1 Uwanja wa Upton Park.

    1992-93: FERGIE ALIPOMALIZA UKAME WA MATAJI WA MIAKA 26 NA KUANZA KULUNDIKA 'NDOO' O.T.

    Steve Bruce celebrates his second goal against Sheffield Wednesday in 1993
    Wekundu hao walipitia kipindi kigumu cha miaka 26 bila taji la Ligi Kuu. Kocha wa United, Sir Alex Ferguson akawasajili Eric Cantona kutoka Leeds katikati ya msimu, katika usajili ambao utaendelea kuwa kihistoria katika soka ya England. United, Villa na Norwich zilikuwa katika mbio kali za taji. Ushindi dhidi ya Norwich Aprili ulifuatiwa na ushindi dhidi ya Sheffield Wednesday Uwanja wa Old Trafford. United ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 hadi dakika za lala salama, lakini ikatoka nyuma na kushinda 2-1, shukrani kwake Steve Bruce mfungaji wa mabao hayo. Hapa, Bruce akishangilia bao lake la ushindi alilofunga dakika ya 97.

    1993-94: TAJI LINGINE KWA MASHETANI WEKUNDU ROBSON AKIRISHA MBAYA...

    Steve Bruce and Bryan Robson celebrate Manchester United's 1994 title triumph
    Eric Cantona, Andrei Kanchelskis, Ryan Giggs na Mark Hughes waliifanya timu ya Ferguson itishe wakati huo. United waliporomoka kidogo, lakini ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu, Man City uliwarejesha barabarani na Wekundu hao wakashinda mechi zao tano za mwisho msimu huo. Mmoja wa washambuliaji waliokuwa kwenye kikosi cha United ni Bryan Robson aliyefanya mambo makubwa kwa ujumla miaka ya 1980. Hapa anainua taji na Steve Bruce mwishoni mwa miaka yake 13 katika timu hiyo.

    1995-96: FERGIE AMBWAGA KEEGAN UNITED IKITWAA TAJI LA 10

    Eric Cantona scores for Manchester United at Newcastle in 1996
    Alan Hansen alitoa msemo maarufu: "Huna lolote na watoto' wakati makinda wa United wanafungwa na Aston Villa katika mechi ya ufunguzi msimu wa 1995-96. United ilikuwa inazidiwa pointi 12 na kikosi cha Kevin Keegan cha Newcastle mwishoni mwa January. Newcastle wakapoteza makali na United wakasimama imara. Picha hii inamuonyesha 'mchawi wa Kifaransa', Eric Cantona akiwafungia wenyeji bao pekee katika ushindi wa 1-0. Cantona na kipa goalkeeper Peter Schmeichel walikuwa katika kiwango cha juu katika miezi ya mwishoni ya msimu huo. Keegan alizodolewa kwa kauli zake dhidi ya Ferguson na United ikatwaa taji la 10 la ligi kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Middlesbrough katika siku ya mwisho.

    1996-97: TAJI LA NNE NDANI MISIMU MITANO, MWANZO WA UTAWALA WA MAN UNITED NA FERGIE

    Manchester United manager Alex Ferguson celebrates after his team beat Liverpool in their vital Premiership clash at Anfield in 1997
    Makinda wa United wakazidi kukomaa na kujiamini kutoka kushinda mfululizo na Mashetani Wekundu wakatetea taji msimu wa 1996-97. Kikosi cha Ferguson kiliwazidi kwa pionti saba wote Arsenal na Newcastle. Ushindi wa ubingwa ukija mwishoni mwa msimu dhidi ya Liverpool, huku Gary Pallister akifunga mabao mawili na Andy Cole moja United wakiua 3-1. Picha hii inamuonyesha Sir Alex Ferguson akishangilia ushindi Uwanja wa Anfield na Msaidizi wake, Brian Kidd. Taji hilo la nne katika misimu mitano ulikuwa mwanzo wa United kutawala soka ya England.

    1998-99: MSIMU MZURI ZAIDI WA MATAJI MATATU KWA MASHETANI WEKUNDU...

    Andy Cole scores against Tottenham in 1999
    Kama kuna msimu babu kubwa kabisa kwa klabu yoyote England, utakuwa wa Manchester United 1998-99 walipotwaa mataji matatu. United ilikuwa inakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa kikosi cha Arsene Wenger, Arsenal, lakini kufungwa kwa The Gunners na Leeds kuliwaachia mwanya United. Wekundu hao walitoa sare na Blackburn na kisha wakatoa nyuma na kuifunga Tottenham  katika siku ya mwisho ya msimu. Hapa Andy Cole akifunga bao la ubingwa.

    1999-2000: UNITED YABEBA TAJI ILE KIBABE HASWA HASWA KWA POINTI 18 ZAIDI

    Teddy Sheringham and Dwight Yorke of Manchester United celebrate Sheringham's equaliser against Arsenal
    United kubeba taji kibabe haswa chini ya Ferguson ilikuwa ni 1999-2000, walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa pointi 18 zaidi. Wakichagizwa na mafanikio ya mataji matatu 1999, United walikuwa moto. Wasiwasi ulikuja tu pale Wekundu hao walipotolewa katika Klabu Bingwa nchini Brazil. Wakati hayo yakitokea, wapinzani wao wote wakapoteza pointi nyumbani wakati wachezaji wa United wakilaumiana wenyewe. Mechi yao ya kwanza ya ligi kucheza waliporejea nyumbani ilikuwa dhidi ya wapinzani wao wa karibu, Arsenal - Teddy Sheringham (pichani) akishangilia bao lake la kusawazisha na Dwight Yorke, katika mechi iliyoisha kwa sare ya 1-1.

    2000-2001: HAKUNA WA KUIZUIA UNITED WEKUNDU HAO WAKITWAA TAJI LA TATU MFULULIZO

    Manchester United celebrate winning the league title in 2001
    United walitwaa tena taji la Ligi Kuu 2000/2001 - wakiizidi kwa pointi 10 Arsenal, licha ya kupoteza mechi zao tatu za mwisho msimu huo. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya United kutwaa mara tatu mfululizo ubingwa wa ligi. Ushindi wa 6-1 dhidi ya Arsenal Februari, siku ambayo Dwight Yorke alifunga mabao matatu, kilikuwa ni kitu cha kukumbukwa msimu huo. Hapa kikosi cha United kikisherehekea ubingwa wa saba wa Ligi Kuu katika miaka tisa, ambao ulidhihirisha umwamba wao England.

    2002-03: MASHETANI WEKUNDU WAIDUWAZA ARSENAL WAKITOKA NYUMA NA KUTWAA UBINGWA

    Paul Scholes scores first goal against Newcastle in 2003
    Arsenal iliiacha kwa pointi nane United ikiwa imebaki miezi mitatu msimu wa 2002-03, lakini United walizinduka na kupambana hadi kuwapiku The Gunners. Wekundu hao walicheza soka ya kuvutia mwishoni mwa msimu huo, na utamu zaidi ulikuwa pale walipoitandika Newcastle 6-2  Aprili. Hii ni picha ya Paul Scholes akifunga bao lake la kwanza kati ya matatu kwa United katika mechi hiyo. Sare ya 2-2 na Arsenal katika mechi iliyofuata iliwafanya United walingane kwa pointi na The Gunners na hatimaye Ferguson akasherehekea ubingwa mwishoni baada ya Arsenal kupoteza pointi mbele ya Bolton na United ikitwaa taji la 15.

    2006-07: UNITED YAREJEA MATAWI YA JUU FERGUSON AKIMGARAGAZA MOURINHO

    Wayne Rooney celebrates scoring for Manchester United at Everton in 2007
    United ilihitaji sana taji la Ligi Kuu msimu wa 2006-07, baada ya kulikosa kwa misimu mitatu. Jose Mourinho wa Chelsea alikuwa ametwaa mataji mawili yaliyopita na walikuwa wapinzani kweli. Mchuano ulikuwa mkali na wakati wote walizidiana kwa pointi chache. Katika moja ya mechi ngumu ilikuwa Uwanja wa Goodison Park, United walipotoka nyuma kwa mabao 2-0 dhidi ya Everton na kushinda 4-2. Hii ni picha Wayne Rooney akishangilia baada ya kuifungia United bao la nne. Wikiendi iliyofuata, United iliwafunga jirani zao, Manchester City, na Chelsea ikatoa sare na Arsenal, hivyo Wekundu hao kubeba taji.

    2007-08: MKALI GIGGS ATIKISA NYAVU UNITED WAKIENDELEZA UTAWALA

    Ryan Giggs scores for Manchester United at Wigan in 2008
    Ulikuwa msimu mwingine wa miujiza, United wakitwaa taji siku ya mwisho kwa mara ya kwanza ndani ya miaka tisa. Kikosi imara cha Arsenal kilikuwa mbele kwenye mbio za ubingwa 2008, lakini United ikawatoa barabarani. Mwishoni mwa msimu, Chelsea nayo ikakamata barabara, ikiwafunga Man United Uwanja wa Stamford Bridge na kuwafikia kwa pointi zikiwa zimebaki mechi mbili. United, ikiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, ilihitaji kushinda mechi zake mbili zilizobaki. Waliifunga West Ham Uwanja wa Old Trafford na baadaye Wigan 2-0 katika siku ya mwisho. Pichani Ryan Giggs akifunga bao gumu la pili, katika siku ambayo alifikia rekodi ya Sir Bobby Charlton kucheza mechi 758 United. Sir Alex Ferguson, ambaye aliserebuka katika mvua uwanjani, alitwaa taji la 10. Akiwa na damu changa za akina Cristiano Ronaldo, Wayne Rooney na Carlos Tevez kikosini, United pia ilitwaa taji la Ligi ya Mabingwa msimu huo.

    2008-09: WAPINZANI WAKUU, LIVERPOOL WAPIGWA UNITED IKITWAA TAJI LA 18

    Federico Macheda celebrates his winner against Aston Villa
    Msimu wa 2008-09 mbio za ubingwa zilikuwa shughuli pevu, huku Liverpool ikiwa katika nafasi nzuri kileleni na United walilazimika kutokea chini kuwapiku. Lakini moto waliorudi nao mwaka mpya vijana wa Ferguson uliwawezesha kubadilisha sura ya ligi. Federico Macheda, kinda wa miaka 17 wakati huo aliyekuwa hajulikani na yeyote Old Trafford alitokea benchi na kufunga bao la ushindi dhidi ya Aston Villa, United ikishinda 3-2  na kuwaengua kileleni Liverpool kwa mara nyingine tena. United walitwaa kwa mara nyingine kwa mara ya tatu mfululizo taji la Ligi Kuu na la 18 jumla, wakifikia rekodi ya Jogoo la Merseysiders. Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa United kuona timu yao inafikia rekodi ya kutwaa mara nyingi ubingwa wa Ligi Kuu ya Liverpool iliyotawala miaka ya 1970 na 1980.

    2010-11: REKODI YAVUNJWA, TAJI LA 19 LAWAFANYA UNITED WAWE WAO TU

    Wayne Rooney scores overhead kick against Manchester City in 2011
    Wakosoaji wengi walikionda kikosi cha Manchester United cha 2010-11 kwamba hakikuwa katika ubora wake, lakini kilimudu kutwaa ubingwa tena, licha ya ushindani mkubwa kutoka kwa klabu mbili za London, Arsenal na Chelsea. Ushindi wa 2-1 kwa United dhidi ya Chelsea Mei ulitosha kuibebesha ubingwa United iliyotoa sare na Blackburn katika mchezo uliofuata. Hii ni picha bao bora lililofungwa na Wayne Rooney kwa tika tak lililowapa ushindi United dhidi ya mahasimu City Uwanja wa Old Trafford. Taji la 19 kwa United lilikuwa ni rekodi nyingine, wakiipiku Liverpool na kuifanya klabu hiyo kuwa yenye mafanikio zaidi katika soka ya England.

    2012-13: CITY NA MANCINI SI LOLOTE KWA FERGIE AKIIONGOZA UNITED KUBEBA TAJI LA 20

    Robin van Persie scores against Manchester City
    Sir Alex Ferguson na United walipania kurejesha taji la Ligi Kuu walilolipoteza mbele ya jirani zao, Manchester City sekunde za mwishoni msimu wa 2011-12. na wamefanikiwa kutimiza azma hiyo baada ya vita ya miezi. Picha hii inamuonyesha Robin van Persie akipiga mpira wa adhabu dakika za lala salama uliowapa bao la ushindi United katika ushindi wa 3-2 dhidi ya City. Van Persie, aliyesajiliwa kutoka Arsenal msimu huu, ndiye amekuwa chachu ya ubingwa wa United katika miezi yake sita ya mwanzoni, na bao lake hili la ushindi katika mechi ya Desemba uliipaisha United kileleni kwa pointi tano zaidi dhidi ya jirani zao. United iliendeleza moto hadi jana kutwaa taji la 20.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HIVI NDIVYO MAN UNITED ILIVYOTWAA MATAJI YOTE 20 YA LIGI KUU ENGLAND NA HAKUNA KAMA FERGUSON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top