• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 30, 2013

  BENTEKE APIGA TATU PEKE YAKE VILLA IKIITANDIKA SUNDERLAND 6-1


  VITA YA KUEPUKA KUSHUKA DARAJA...

  Bottom six
  TMSHAMBULIAJI Christian Benteke amezidi kumuweka katika wakati mgumu kocha Mtaliano, Paolo Di Canio baada ya usiku wa jana kufunga mabao matatu katika ushindi wa Aston Villa wa 6-1 kwenye Uwanja wa  Villa Park katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Ushindi huo umempa ahueni kocha Paul Lambert na kikosi chake kwa kujiondoa kwenye wasiwasi wa kushuka Daraja.
  Benteke alifunga mabao yake katika dakika za 55, 59 na 72, wakati mabao mengine ya Villa yalitiwa kimiani na Vlaar dakika ya 31, Weimann dakika ya 38 na Agbonlahor dakika ya 88. Bao pekee la Sunderland lilifungwa na Danny Rose dakika ya 32.
  Kikosi cha Villa kilikuwa; Guzan, Vlaar, Bennett, Baker, Lowton, Westwood, Delph, Sylla, Agbonlahor, Benteke/Bent, dk79 na Weimann.
  Sunderland: Mignolet, Bardsley, O'Shea, Cuellar, Rose, N'Diaye, Larsson/McClean dk61, Gardner/Vaughan dk86,  Johnson, Sessegnon, Graham/Mandron dk85.
  Matchwinner: Christian Benteke's hat-trick gave Aston Villa a vital victory over Sunderland
  Mshindi wa mechi: Christian Benteke akishangilia Hat-trick yake iliyoipa Villa ushindi mnene dhidi ya Sunderland
  The equaliser: But Danny Rose's goal had suggested this wouldn't be such a one-sider affair
  La kufutia machozi: Danny Rose akishangilia bao lake ambalo lilikuwa la kusawazisha, lakini mwishowe wakalala 6-1
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BENTEKE APIGA TATU PEKE YAKE VILLA IKIITANDIKA SUNDERLAND 6-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top