• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 21, 2013

  YANGA NA JKT RUVU ILIKUWA TAMU AJE LEO...HIVI NDIVYO WATOTO WA JANGWANI WALIVYOPELEKA POSA YA MWALI

  Beki wa JKT Ruvu, Stanley Nkomola akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Yanga SC, Simon Msuva katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-0.

  Utamu wa bao; Nizar Khalfan akishangilia bao lake la tatu aliloifungia Yanga leo

  Kipa wa JKT Ruvu, Shaaban Dihile akidaka mpira wa juu

  Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akifuarahia baada ya krosi yake kuzaa bao

  Mkamate kama unaweza; Msuva akiambaa na mpira dhidi ya Damas Makwaya wa JKT

  Mabingwa watarajiwa; Kikosi cha Yanga SC leo

  Kikosi cha JKT Ruvu leo

  Katikati ya dimba; Kiungo wa Yanga, Frank Domayo akimdhibiti kiungo wa JKT Ruvu mbele yake

  Yanga TV; Shabiki wa Yanga akiwa na kitu mfano wa kamera

  Hunitishi; Simon Msuva wa Yanga akizozana na Haroun Adolph wa JKT Ruvu

  Kombe bandia; Mashabiki wa Yanga wakishangilia na Kombe la 'kubumba'

  Kwa raha zao; Mashabiki wa Yanga, cheki huyo ambaye yuko na mtoto wake, anamuambukiza maradhi mapemaaa

  Anachungulia; Haruna Niyonzima akijiandaa kupiga krosi iliyozaa bao la tatu

  Busu motomoto; Nahodha wa Yanga, Nador Haroub 'Cannavaro' akimpiga busu Simon Msuva baada ya kufunga

  Simon Msuva akimpongeza Hamisi Kiiza kufunga bao la pili

  Amewanyonga; Msuva akiwakebehi mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia JKT Ruvu baada ya kufunga

  Mwanariadha?Msuva akikimbia kushangilia bao lake 

  Athumani Iddi 'Chuji' akimiliki mpira mbele ya kiungo wa JKT Ruvu,  Nashon Naftali, huku Haruna Niyonzima akiwa tayari kutoa msaada 

  David Luhende wa Yanga akimtoka Hassan Kikutwa wa JKT Ruvu

  Nizar Khalfan akichanja mbuga... 

  Hawa vipi? Kipa Shaaban Dihile nyuma akiwa amenagukiwa na beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' katika moja ya hekaheka za mechi hiyo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: YANGA NA JKT RUVU ILIKUWA TAMU AJE LEO...HIVI NDIVYO WATOTO WA JANGWANI WALIVYOPELEKA POSA YA MWALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top