• HABARI MPYA

    Friday, April 12, 2013

    NI WIKIENDI YA KUFA MTU LIGI KUU BONGO, YANGA, SIMBA NAA ZAM MZIGONI DAR

    Yanga SC; Itabakia kileleni baada ya mechi za wikiendi?

    Na Boniface Wambura
    LIGI Kuu ya Vodacom inaendelea kesho (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
    Yanga itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting.
    Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Aprili 14 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zaje 49, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 46, Kagera Sugar 37 na Simba SC 35.
    Mchezo wa Jumapili unatarajiwa kutoa taswira nzima ya Ligi Kuu msimu huu, kwani iwapo SImba SC itashinda, Yanga ikishinda kesho itapiga hatua kubwa katika mbio zake za ubingwa.
    Simba SC imedhamiria kushinda Jumapili, ili kuweka hai matumaini ya japo kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ili ipate nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho.
    Simba SC iliingia kambini katika hoteli ya Bamba Beach, KIgamboni, Dar es Salaam tangu jana kujiandaa na mchezo huo, wakati Azam ipo maskani kwake, Chamazi, Dar es Salaam. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NI WIKIENDI YA KUFA MTU LIGI KUU BONGO, YANGA, SIMBA NAA ZAM MZIGONI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top