• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 27, 2013

  KIFAA CHA BRAZIL KUANZA KAZI MAN UNITED MUDA SI MREFU

  United front: Wellington Bueno (right) is set to start pre-season wat Old Trafford
  Wellington Bueno (kulia) anajaindaa kuanza maandalizi ya msimu mpya Old Trafford  KLABU ya Manchester United inatarajiwa kuanza maandalizi ya msimu mpya na kiungo wa Desportivo Brasil, Wellington Bueno. 
  Kinda huyo wa umri wa miaka 17, ambaye amekuwa akifananishwa na Mchezaji Bora wa zamani wa dunia, Kaka, amekuwa akifanya mazoezi na FC Twente.
  Wellington, ambaye pia anakwenda kwa jina la Juninho, ni sehemu ya programu ya United kuendeleza vipaji vya chipukizi Amerika Kusini. 
  Wachezaji wengine ni pamoja na Bruno Gomes, mshambuliaji, na Lucas Evangelista, ambaye anacheza kwa mkopo kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 cha Sao Paolo. Mwingine, Agnaldo, yupo na mshambuliaji wa zamani wa United, Ole Gunnar Solskjaer nchini Norway.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KIFAA CHA BRAZIL KUANZA KAZI MAN UNITED MUDA SI MREFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top