• HABARI MPYA

    Saturday, April 27, 2013

    WENGER AMFANANISHA VAN PERSIE NA MWANAMKE ALIYETAKA KUWA MGUMBA NA AMWAMBIA; "HUWEZI KUWA MCHEZAJI BORA ENGLAND"

    FADHILA nzuri ambazo kocha Arsene Wenger anaweza kulipa kwa Robin van Persie ilikuwa ni kumfananisha na mwanamke aliyechelewa kupata mtoto hadi umri wa miaka 39.
    Si hivyo tu, lakini Wenger hafikirii kama nyota huyo mwenye mabao 24 anastahili tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA na Michael Carrick ndiye chaguo la kocha huyo wa Arsenal.
    "Wakati fulani si tu mfungaji apewe tuzo, bali mchezaji halisi katika moyo wa mchezo,"alisema Wenger, ambaye amesema watawapa heshima yao Manchester United katika mchezo wa kesho.
    Hungry: Robin van Persie had not enjoyed success at Arsenal for several years
    Hasira: Robin van Persie hajapata mafanikio akiwa Arsenal kwa miaka kadhaa

    "Carrick, kwangu, anastahili hii. Anatoa pasi bora. Anaweza kucheza Barcelona. Anaweza kuendana na mchezo wao."
    Van Persie kesho atarejea Arsenal kwa mara ya kwanza tangu ahamie Old Trafford. Matunda ya kuondoka kwake Arsenal na kutua United yameanza kuonekana baada ya kuiwezesha timu hiyo kurudisha ubingwa wa Ligi Kuu.
    Bitter? Arsene Wenger said that Van Persie should not be player of the year
    Chuki? Arsene Wenger amesema Van Persie hastahili kuwa mchezaji bora wa mwaka

    Alipoulizwa kama alijua Van Persie atakwenda 'kulipa' Old Trafford, Wenger alionekana kuhamaki, kabla ya kusema: "Ndiyo! Tusingeweza kushindana kwa sababu ilikuwa  imekwishakaa vibaya.
    "Ni kijana mkweli, Robin. Amefikisha miaka 29 na alifikiri, “Tunaweza kutwaa ubingwa hapa au ninaweza kuwa na nafasi sehemu nyingine pia?” Kuna wakati mgumu kama ambao anaweza kukutana nao mwanamke ambaye katika umri wa miaka 39 hajapata mtoto. Ataanza kufikiri, “Sina muda zaidi”.’
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WENGER AMFANANISHA VAN PERSIE NA MWANAMKE ALIYETAKA KUWA MGUMBA NA AMWAMBIA; "HUWEZI KUWA MCHEZAJI BORA ENGLAND" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top