• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 28, 2013

  LEWANDOWSKI KUTUA MAN UNITED, FERGUSON APANGA ACHEZE PACHA NA VAN PERSIE...WATATISHAA MBAYAA


  KLABU ya Manchester United itajaribu kupambana na klabu za Ujerumani, Bayern Munich na Borussia Dortmund kuwania saini ya mshambuliaji wa Dortmund, Robert Lewandowski mwenye thamani ya Pauni Milioni 25. 
  Sir Alex Ferguson, ambaye amekuwa akimfuatilia Lewandowski kwa miezi 18, ana matumaini mapya ya kumnasa mpachika mabao huyo wa Poland, ambaye alifunga mabao yote manne dhidi ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki hii. 
  United wakati wote inahofia Lewandowski, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake atahamia Bayern na taarifa zinasema amesaini mkataba wa awali wa makubaliano. 
  Star man: Borussia Dortmung striker Robert Lewandowski (centre) is one of Europe's hottest properties
  Nyota: Mshambuliaji wa Borussia Dortmung, Robert Lewandowski (katikati) ni miongoni mwa wachezaji gumzo Ulaya

  Lakini, klabu hizo za Ujerumani zikiwa katika uwezekano kukutana kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Wembley baada ya kushinda vizuri mechi za kwanza za Nusu Fainali nyumbani dhidi ya Barcelona na Madrid, upinzani wao unaweza ukahusika katika uhamisho wa mchezaji huyu. 
  Tayari mashabiki wa Dortmund wana hasira za kiungo wao, Mario Gotze kukubali kuhamia Bayern mwishoni mwa msimu baada ya kufikia makubaliano ya Pauni Milioni 23 na ikiwa Lewandowski atamfuata mwenzake, inaweza kuwa balaa. 
  Ferguson anapanga Lewandowski akacheze pamoja na Robin van Persie.
  Alisema: "Mashabiki wa Dortmund hawawezi kufurahia kilichotokea. Sifikiri kama klabu itamuuza Lewandowski kwa Bayern. Nafikiri wataamua amalizie mkataba wake au wamuuze sehemu nyingine. 
  Destructive: Lewandowski was sensational against Real Madrid last week, scoring four times
  Anatisha kama njaa: Lewandowski alikuwa kila kitu dhidi ya Real Madrid wiki hii akifunga mabao manne
  Destructive: Lewandowski was sensational against Real Madrid last week, scoring four times
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: LEWANDOWSKI KUTUA MAN UNITED, FERGUSON APANGA ACHEZE PACHA NA VAN PERSIE...WATATISHAA MBAYAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top