• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 29, 2013

  WENGER ACHARUKA, AMUAMBIA FERGUSON; "HUPATI TENA MCHEZAJI ARSENAL"


  KOCHA Arsene Wenger amesema kwamba hatauza mchwezaji wake yeyote mwingine wa Arsenal kwenda Manchester United, baada ya Robin van Persie kutimka Emirates kuhamia Old Trafford msimu huu.
  Mholanzi huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha United kilichotoa sare ya 1-1 na Arsenal jana mjini London baada ya kutolewa salamu ya heshima na wachezaji wenzake wa zamani kwa ubingwa. 
  Mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu England alizomewa na mashabiki wa timu yake ya zamani ambao walikuwa wakimshangilia enzi zake Arsenal, lakini akafunga kwa penalti kuisawazishia United baada ya Theo Walcott kutangulia kufunga mapema. 
  Returning: Robin van Persie (right) was back at the Emirates after leaving Arsenal for Manchester United
  Aliporejea: Robin van Persie (kulia) alirejea Emirates kwa mara ya kwanza jana tangu alipotimkia Manchester United

  Wenger aliyemuuza kwa Pauni Milioni 24 Van Persie, aliyefunga mabao 37 katika mashindano yote The Gunners, alipoulizwa iwapo mpinzani wake namba moja, Sir Alex Ferguson akitaka wachezaji zaidi kwake, alijibu: "Sifahamu, lakini hatasajili kwetu,".
  Arsenal imebakiza mechi tatu na ina matumaini ya kuwapiku wapinzani Tottenham na Chelsea kupata nafasi katika Nne Bora ya Ligi Kuu England ili kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
  No deal: Arsene Wenger (right) says he will not sell another player to Sir Alex Ferguson
  Hupati kitu tena: Arsene Wenger (kulia) amesema hatauza mchezaji wake mwingine yeyote kwa Sir Alex Ferguson
  Defiant: Arsene Wenger says none of his Arsenal players will follow the Dutchman to Manchester United
  Hasira: Arsene Wenger amesema hakuna tena mchezaji wa Arsenal atakayemfuata Mholanzi Manchester United
  Frosty: Van Persie was jeered by Arsenal fans throughout his return
  Cheki kitu hicho: Van Persie alizomewa na mashabiki wa Arsenal
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WENGER ACHARUKA, AMUAMBIA FERGUSON; "HUPATI TENA MCHEZAJI ARSENAL" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top