• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 20, 2013

  SIR FERGUSON AMWAMBIA ROONEY; HUNA NAMBA TENA MAN UNITED


  KOCHA Sir Alex Ferguson amemuonya Wayne Rooney kwamba hana tena uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza cha Manchester United.
  Baada ya kumchezesha katika nafasi ya kiungo kwa mechi ya pili dhidi ya West Ham Jumatano usiku na kumtoa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kipindi cha pili, Ferguson amesema atafanya hivyo tena.
  Kaangalie video chini
  No go: Wayne Rooney will not join PSG in the summer, according to Sir Alex Ferguson
  Hakuna kwenda: Wayne Rooney hatajiunga na PSG mwishoni mwa msimu kwa mujibu wa Sir Alex Ferguson
  Off you go: Rooney rubs his face as he walks off the pitch to be substituted against West Ham
  Anakwenda benchi: Rooney akiinamisha sura yake wakati anatoka uwanjani alipotolewa dhidi ya West Ham
  Rooney yupo katika wakati mgumu kwa kuchezeshwa kwenye nafasi isiyo yake na haijulikani mustakabali wake utakuwaje Old Trafford ikiwa atasaini mkataba mpya mwishoni mwa msimu.
  Majadiliano yanatarajiwa kufanyika Ligi Kuu England itakapomalizika juu ya mkataba mpya.
  Rooney amekuwa akihusishwa na kuhamia Paris Saint-Germain, lakini Ferguson amepuuza tetesi hizo jana akisema: "Sifikiri kama kuna lolote katika hilo hata kidogo.’ 
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIR FERGUSON AMWAMBIA ROONEY; HUNA NAMBA TENA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top