• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 21, 2013

  SUAREZ AIOKOA LIVERPOOL KUZAMA KWA CHELSEA, AMNG'ATA IVANOVIC


  BADO kifogo tu kocha wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez aibuke na ushindi katika mechi yake ya kwanza dhidi ya timu yake hiyo ya zamani Uwanja wa Anfield, lakini mshambuliaji wa Wekundu hao, Luis Suarez akazima ndoto hizo kwa kufunga bao la kusawazisha dakika za lala salama.
  Oscar alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 26, lakini Strurridge akasawazisha dakika ya 52 kabla ya Hazard  kuifungia The Blues bao la pili kwa penalti dakika ya 57 na Suarez akasawazisha dakika ya 90. 
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Reina, Johnson, Carragher, Agger, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Downing/Shelvey dk80, Henderson, Coutinho/Sturridge dk46 na Suarez.
  Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Bertrand, Ramires, Mikel, Mata/Lampard dk90, Oscar/Moses dk83, Hazard/Benayoun dk78 na Torres.

  At the death: Luis Suarez headed in a late equaliser to rescue a point for Liverpool against Chelsea
  Rufaa ya kifo: Luis Suarez akifunga kwa kichwa bao la kusawazisha kwa timu yake Liverpool dhidi ya Chelsea
  Hungry? Suarez appeared to bite Chelsea's Branislav Ivanovic during the second half
  Njaa? Suarez alimuuma Branislav Ivanovic kipindi cha pili.
  Opener: Oscar headed Chelsea into the lead midway through the first half at Anfield
  Bao la kwanza: Oscar akiifungia Chelsea bao la kwanza kwa kichwa Uwanja wa Anfield
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SUAREZ AIOKOA LIVERPOOL KUZAMA KWA CHELSEA, AMNG'ATA IVANOVIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top