• HABARI MPYA

    Thursday, April 18, 2013

    RAIS JK, DK BILAL WAONGOZA MAZISHI YA BI KIDUDE, DIAMOND ALIKUWEPO HADI MSIKITINI KUSHIRIKI IBADA

    Maelfu ya wananchi na waumini wa dini ya kiislamu waliofurika katika msikiti wa Mwembeshauri katika maziko ya Marehemu Bikidude leo, wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa marehemu huyo wakati wakielekea mazikoni kijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati Unguja.
    Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika maziko ya marehemu Bi Fatma Baraka 'Kidude'  kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Kati Unguja.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la Msanii mkongwe wa Muziki wa Mwambao (Taarab) Tanzania,Marehemu Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo mchana.

    Rais wa  jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kuli) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(kulia waliokaa) Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif, na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,wakiomba dua baada ya maziko ya Msanii maarufu Fatma Binti Baraka 'Kidude' aliyefariki jana na kuzikwa leo Kijijini kwao Kitumba,Wilaya ya Kati Unguja.

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mohammed Ali Mohamed Shein, wakishiriki katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja.Picha na OMR
     Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ramadhan Nasib (kulia)'Diamond Plutnum', akiwa ni mmoja kati ya wasanii waliohudhuria katika dua maalum ya kumswalia marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude', iliyofanyika mchana huu katika Msikiti wa Mwembeshauri, mjini Zanzibar. Bi Kidude anatarajia kuzikwa mchana huu kijijini kwao  Kitumba Wilaya ya Kati, Unguja. Picha na OMR.
    Waumini wa dini ya Kiislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Fatma Baraka 'Bi Kidude'(picha ndogo juu kushoto), wakati wakiingiza jeneza hilo Msikiti wa Mwembeshauri, kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya kuelekea kijijini kwa marehemu, Kitumba Wilaya ya Kati kwa maziko, mchana huu. Picha na OMR
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: RAIS JK, DK BILAL WAONGOZA MAZISHI YA BI KIDUDE, DIAMOND ALIKUWEPO HADI MSIKITINI KUSHIRIKI IBADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top