• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 30, 2013

  MTANZANIA APEWA ITC KUCHEZA MSUMBIJI

  Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kushoto, wanacheza DRC. Idadi ya Watanzania wanaocheza nje yazidi kuongezeka

  Na Boniface Wambura
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Yussuf Kunasa kucheza nchini Msumbiji.
  Shirikisho la Soka Msumbiji (FMF) lilituma maombi TFF kumuombea hati hiyo Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya Estrela Vermelha da Beira inayocheza Ligi Kuu nchini humo.
  Kunasa ambaye msimu huu hakuwa na timu, amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji wa ridhaa. 
  Zaidi ya wachezaji 10 kutoka Tanzania hivi sasa wanacheza katika klabu mbalimbali nchini Msumbiji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MTANZANIA APEWA ITC KUCHEZA MSUMBIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top