• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 22, 2013

  DROGBA NA ETO'O WATENGEWA TUZO AMBAYO MESSI HATII MGUU

  Drogba kulia na Eto'o kushoto; Tuzo hii Messi hatii mguu kwa sababu bado kinda

  Na Naseem Mahmoud
  WASHAMBULIAJI bora kuwahi kutokea barani Afrika, Didier Drogba na Samuel Eto’o wameingizwa kwenye orodha ya kuwania tuzo ya Guu la Dhahabu mwaka 2013, kufuata nyayo za mshambuliaji wa Paris Saint Germain ya Ufaransa, Zlatan Ibrahimovic, aliyeshinda mwaka jana.
  Manahodha hao wa Ivory Coast na Cameroon ni Waafrika pekee katika orodha ya wachezaji tisa walioingizwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzi hiyo, inayotolewa kwa wachezaji wenye mafanikio makubwa na mwonekano mzuri.
  Wawania tuzo hiyo wengine ni Mfaransa David Trezeguet, Mjerumani Miroslav Klose, Mtaliano Andrea Pirlo, Waspanyola Andres Iniesta na Iker Casillas na Waingereza Franck Lampard na David Beckham.
  Tuzo huyo Guu la Dhahabu inatolewa kwa mchezaji aliye uwanjani ambaye angalau ana umri usiopungua miaka 29 na hawezi kushinda zaidi ya mara moja
  Washindi wa awali wa tuzo hiyo ni; 2003: Roberto Baggio (Italia, Brescia) 2004: Pavel Nedved (Jamhuri ya Czech, Juventus) 2005: Andryi Shevchenko (Ukraine, AC Milan) 2006: Ronaldo (Brazil, Real Madrid) 2007: Alessandro Del Piero (Italia, Juventus) 2008: Roberto Carlos da Silva (Brazil, Fenerbahçe) 2009: Ronaldinho (Brazil, AC Milan) 2010: Francesco Totti (Italia, Roma) 2011: Ryan Giggs (Wales, Manchester United) na 2012: Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris SG).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: DROGBA NA ETO'O WATENGEWA TUZO AMBAYO MESSI HATII MGUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top