• HABARI MPYA

    Saturday, April 20, 2013

    ARSENAL YARUDI TATU BORA LIGI KUU ENGLAND BAADA YA KUIBWAGA FULHAM 1-0


    KLABU ya Arsenal imerejea katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fulham kwenye Uwanja wa Craven Cottage katika mchezo ambao kila timu ilipoteza mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu.
    Fulham wanaweza kujihesabu hawakuwa na bahati kwa kushindwa japo kuondoka na pointi moja kwenye mechi hiyo baada ya kutolewa mapema kwa kiungo Steve Sidwell - ambaye alikuwa anarejea uwanjani baada ya kumaliza adhabu ya mechi tatu kwa kumchezea rafu Mikel Arteta dakika ya 12.
    Arsenal ilitumia mwanya huo kujipatia bao pekee la ushindi dakika ya 43 lililotiwa kimiani na beki Per Mertesacker kwa kichwa kabla ya Olivier Giroud kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 90 kwa kumchezea rafu Stanislav Manolev.
    Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Rosicky/Podolski dk71, Arteta, Ramsey, Walcott/Wilshere dk71, Giroud na Cazorla/Vermaelen dk90.
    Fulham: Schwarzer, Manolev, Senderos, Hangeland, Richardson, Emanuelson/Frei dk87, Sidwell, Enoh, Kacaniklic/Petric dk85, Ruiz na Berbatov.

    High five: Per Mertesacker (left) celebrates scoring the opening goal with Nacho Monreal
    Chukua gwala: Per Mertesacker (kushoto) akishangilia bao lake pekee la ushindi na Nacho Monreal
    Heading home: Arsenal's Per Mertesacker slides in to score Arsenal's goal from a yard out
    Kitu nyavuni: Beki wa Arsenal, Per Mertesacker akiteleza kufunga kwa kichwa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL YARUDI TATU BORA LIGI KUU ENGLAND BAADA YA KUIBWAGA FULHAM 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top