• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 21, 2013

  SPURS WAIBUTUA MAN CITY 3-1 NA KUITENGEA UBINGWA MAN UNITED MAPEMAAAAAA

  KLABU ya Tottenham imefufua matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kuitandika mabao 3-1 Manchester City na kuwakatisha tamaa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England.
  Kiungo wa zamani wa Arsenal, Samir Nasri aliifungia bao la kuongoza Man City dakika ya tano, lakini baada ya hapo vijana wa Andre Villas-Boas wakaigeuzia kibao City.
  Clint Dempsey aliisawazishia Spurs dakika ya kabla ya 57 Jermain Defoe kufunga la pili dakika ya 79 na Gareth Bale kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la City dakika ya 82.
  Matokeo hayo yanamaanisha Manchester United wanaweza kujihakikishia ubingwa kesho wakishinda, kwani watafikisha pointi 84 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
  Kikosi cha Tottenham Hotspur kilikuwa; Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Assou-Ekotto, Sigurdsson/Holtby dk60, Dembele, Parker/Huddlestone dk61, Bale, Dempsey na Adebayor/Defoe dk71.
  Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy/Lescott dk90, Toure, Barry, Milner/Kolarov dk46, Tevez, Nasri na Dzeko/Sinclair dk82.
  That'll do it: Gareth Bale dinks the ball over Joe Hart to make it 3-1 and complete the comeback
  Kitu hicho: Gareth Bale akimtungua Joe Hart na kufanya 3-1
  Cracker: Jermain Defoe curls home Tottenham's second goal, as Vincent Kompany looks on helpless
  Shuti: Jermain Defoe akiifungia Tottenham bao la pili mbele ya Vincent Kompany
  Revival: Clint Dempsey celebrates the first of three Tottenham goals in seven minutes against Man City
  Ufufuko: Clint Dempsey akishangilia bao la kusawazisha aliloifungia Tottenham
  FA Premier League - Top Six (before Chelsea game)
  Sita Bora ya Ligi Kuu England kabla ya matokeo ya Chelsea na Liverpool
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SPURS WAIBUTUA MAN CITY 3-1 NA KUITENGEA UBINGWA MAN UNITED MAPEMAAAAAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top