• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 20, 2013

  AKINA NDITI WATINGA FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND BAADA YA KUIKUNG'UTA LIVERPOOL NJE NDANI


  TIMU ya vijana ya Chelsea imetinga Fainali ya Kombe la FA la Vijana kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya mabao ya John Swift dakika ya 40 na Nathan Ake dakika ya 45+1 kuwaua wapinzani, Liverpool.
  Tayari mabao mawili ya Alex Kiwomya katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Stamford Bridge yaliifanya Chelsea iingine kifua mbele uwanjani jana, na hata Kristoffer Peterson alipoifungia bao moja Liverpool dakika ya 13 jana, lilionekana la kufutia machozi tu. 
  Kiungo Mtanzania wa Chelsea U18 ambayo sasa itamenyana na Norwich City katika fainali, Adam Nditi jana kwa mara ya pili mfululizo hakuwemo kabisa kwenye kikosi cha timu hiyo.
  Katika mchezo wa jana, kikosi cha Chelsea kilikuwaMitchell Beeney, Ola Aina, Alex Davey, Nathan Ake/Dion Conroy dk84, Kevin Wright, Lewis Baker, Alex Kiwomya, Ruben Loftus-Cheek, Islam Feruz/Charlie Colkett dk77, John Swift/Connor Hunte dk53 na Jeremie Boga.
  Liverpool: Ryan Fulton, Yalany Baio, Joe Maguire, Lloyd Jones, Danny Cleary, Jordan Lussey, Jack Dunn/Alex O’Hanlan dk84, Jordan Rossiter/Nathan Burke dk78, Jerome Sinclair, Dan Smith na Kristoffer Peterson.
  Into the final: Chelsea celebrate getting to the final of the FA Youth Cup for the second year in a row
  Safari fainali: Chelsea wakishangilia jana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AKINA NDITI WATINGA FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND BAADA YA KUIKUNG'UTA LIVERPOOL NJE NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top