• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 24, 2013

  CHELSEA ASILIMIA 99.9 WAMEMPATA FALCAO NA WAMEAMUA KUACHANA NA CAVANI


  KLABU ya Chelsea inaamini imeshinda mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Radamel Falcao.
  Mazungumzo na wawakilishi wa nyota huyo wa Colombia na viongozi wa Atletico yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa sasa, lakini Chelsea wanafikiri wako karibu kumsajii.
  BIN ZUBEIRY kwa msaada wa Sportsmail inaweza kuweka bayana kwamba, klabu hiyo ya London imeachana na mpango wa muda mrefu wa kumsajili Edinson Cavani na kuongeza nguvu katika kuwania saini ya Falcao.
  We've got our man: Chelsea believe they are on the verge of completing a deal for Radamel Falcao
  Tumempata mtu wetu: Chelsea inaamini iko karibu sana kumnasa Radamel Falcao
  On target: Falcao celebrates scoring against Sevilla in a La Liga match on Sunday
  Amefunga: Falcao akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Sevilla kwenye La Liga Jumapili
  On target: Falcao celebrates scoring against Sevilla in a La Liga match on Sunday
  Roman Abramovich ameridhia kumpa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki mchezaji huyo na pia atatoa kiasi cha Pauni milioni 46 ambazo Atletico inataka kama dau la kumuuza nyota wake huyo.
  Kipa wa Chelsea, Thibault Courtois yuko ndani ya mazungumzo ya uhamisho. Mbelgiji huyo amekuwa kivutio akicheza kwa mkopo wa muda mrefu Atletico na klabu hiyo ya Hispania inataka kuendelea na kipa huyo mwenye umri wa miaka 20.
  Timu ya makocha wa Chelsea, inaamini Courtois atanufaika kutoka kwa kucheza kwa mkopo na kurudi Ligi Kuu England msimu ujao, wakiwa wamemuandaa kurithi mikoba ya Petr Cech. 
  Lakini wako tayari kumuacha kwa msimu mwingine katika Jiji la Madrid, ili wamtumie kipa huyo kama chambo cha kumnasa Falcao.
  Chelsea ilikuwa inamtaka sana Falcao, mwenye umri wa miaka 27 na kama itamkosa ilipanga kuhamishia ndoana zake kwa Cavani, mwenye umri wa miaka 26. Nyota huyo wa Uruguay amekuwa kipenzi cha mmiliki wa Chelsea, Abramovich na Mkurugenzi wa Ufundi, Michael Emenalo.
  Wawakilishi wa mshambuliaji huyo wa Napoli hivi karibuni walizungumza na viongozi wa Chelsea juu ya uhamisho wa mwishoni mwa msimu, kuonyesha kwamba Stamford Bridge yangekuwa maskani mapya ya Cavani akihamia England.
  Lakini pamoja na Chelsea kuamua kuelekeza nguvu zao kwa Falcao, pia wanamuwania mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle, mwenye umri wa miaka 22.
  Wakati huo huo, Nahodha John Terry anatumai kuanza mazungumzo ya mkataba mpya mwishoni mwa msimu. Beki huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye maisha yake yote ya soka amekuwa Stamford Bridge, anamaliza mkataba wake msimu ujao.
  Central role: Atletico Madrid's goalkeeper Thibaut Courtois, on loan from Chelsea, is key to negotiations
  katikati ya dili: Kipa wa Atletico Madrid, Thibaut Courtois, yupo kwa mkopo kutoka Chelsea, ni sehemu ya mazungumzo ya uhamisho wa Falcao
  Pulled out: Chelsea have passed up the opportunity to negotiate with Napoli striker Edinson Cavani
  Wameachana naye: Chelsea imeachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani
  Andre Schurrle
  Andre Schurrle
  Kifaa kuelekea darajani: Chelsea imepiga hatua katika mazungumzo yake na nyota wa Bayer Leverkusen, Andre Schurrle
  .New contract? John Terry's current Chelsea deal expires at the end of next season
  Mkataba mpya? John Terry mkataba wake wa sasa Chelsea  unaisha msimu ujao
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CHELSEA ASILIMIA 99.9 WAMEMPATA FALCAO NA WAMEAMUA KUACHANA NA CAVANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top