• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 22, 2013

  YANGA NA JKT RUVU JANA MILIONI 66 MAPATO

  Nyota wa mechi ya jana, Simon Msuva kushoto akijaribu kumtoka beki wa JKT Ruvu 

  Na Boniface Wambura
  MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya JKT Ruvu na Yanga iliyochezwa jana (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,568,000 kutokana na watazamaji 11,864.
  Viingilio katika mechi hiyo namba 106 iliyomalizika kwa Yanga kutoa dozi ya 3-0 kwa wenyeji wao vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,702,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,154,440.68.
  Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,984,450.40, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,790,670.24, Kamati ya Ligi sh. 4,790,670.24, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,395,335.12, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 931,519.21 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 931,519.21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: YANGA NA JKT RUVU JANA MILIONI 66 MAPATO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top