• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 29, 2013

  AZAM WAANZA SAFARI YA SAA TISA ANGANI KUISAKA CASSABLANCA

  Wachezaji wa Azam FC, Himid Mao na John Bocco 'Adebayor' nyuma yake wakiwa kwenye foleni ya kuingia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai, Falme za Kiarabu asubuhi hii tayari kupanda ndege ya Shirika la Emirates kwenda Morocco kucheza na wenyeji FAR Rabat katika mchezo wa marudiano, Kombe la SHirikisho Afrika Raundi ya Tatu Jumapili. Azam iliyotoa sare ya 0-0 Dar es Salaam, ililala hapa jana ikitokea Dar es Salaam. 

  Beki wa Azam FC, David Mwantika akikaguliwa pasipoti yake na wafanyakazi wa Emirates Dubai leo. Azam watasafiri kwa saa tisa kuanzia saa 1:35 za hapa sawa na 12: 35 za Dar es Salaam kuelekea Cassablanca.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AZAM WAANZA SAFARI YA SAA TISA ANGANI KUISAKA CASSABLANCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top