• HABARI MPYA

    Wednesday, April 18, 2012

    SIMBA SC YATAFUNA AFANDE LA JESHI, YANGA YAKALISHWA KAITABA

    Gervais Kago kulia, Patrick Mafisango katikati na Uhuru Suleiman kushoto wakishangilia leo
    Kago akimtoka beki wa JKT
    Haruna Moshi 'Boban' akimtoka kiungo wa JKT

    NDOTO za Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania zinaanza kutimia baada ya jana kuichapa JKT Ruvu kwa mabao 3-0  katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaamm jioni hii, bongostaz.blogspot.com inakuletea taarifa.
    Kwa matokeo hayo, Simba imejiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa huo baada ya kujikita zaidi kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 56 ikiwazidi, pointi 13 mabingwa watetezi, Yanga.
    Simba ilianza kwa kasi mchezo na kufanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya kwanza ya mchezo lililofungwa na Uhuru Selemani kwa kichwa baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na Emnuel Okwi.
    Simba walizidi kulisakama lango la JKT Ruvu ambapo katika dakika ya saba, Amir Maftah alitoa pasi ambayo   Seleman  alichelewa kuunganisha na kutoka nje.
    Simba waliendelea kulisakama lango la JKT ambapo katika dakika ya 17, Haruna Moshi ‘Boban’ aliipatia timu yake bao la pili baada ya uzembe uliofanywa na Emanuel Pius wa JKT na kupachika wavuni mpira.
    Wekundu hao wa Msimbazi, walifanya mashambulizi tena katika dakika ya 26 ambapo Seleman alikosa bao baada ya kupaisha juu mpira  aliopasiwa na Maftah huku Gervas Kago naye akikosa akikosa bao baada ya kushindwa kumalizia pasi ya Seleman katika dakika ya 39.
    JKT walicharuka na kuliandama lango la Simba ambapo katika dakika ya 42, Hussein Bunu  alikosa bao baada ya kushindwa kumalizia pasi ya Pius.
    Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kusaka bao, lakini katika dakika ya 64, Mwinyi Kazimoto aliipatia Simba bao la tatu baada ya kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa JKT, Aman Simba.
    JKT walifanya mabadiliko katika dakika ya 71 kwa kutoka Mohamed Banka na nafasi yake kuchukuliwa na  George Mketo.
    Kwa upande wa Simba alitoka Juma Nyoso na kuingia Obadia Mungusa, huku Kago akitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Edawrd Christopher.
    Mashabiki wa Simba kwa raha zao taifa leo
    Katika mchezo mwingi wa ligi hiyo uliochezwa uwanja wa Kaitaba, Bukoba, timu ya Kagera Sugar iliifunga Yanga bao 1-0 lililofungwa na Shijja Hassan Mkina katika dakika ya 30.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YATAFUNA AFANDE LA JESHI, YANGA YAKALISHWA KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top