• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 25, 2012

  LAMPARD AWAPONGEZA WENZAKE, ASEMA YEYOTE AJE IWE REAL AU BAYERN WAKO TAYARI


  CL - FC Barcelona v FC Chelsea, Frank Lampard
  Getty Images
  KIUNGO wa Chelsea, Frank Lampard amewapongeza wachezaji wenzake baada ya Chelsea kutoka nyuma mbele ya Barcelona na kushinda kwa jumla ya mabao 3-2 na kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa.

  The Blues walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 katika usiku huu kabla ya kumpoteza nahodha wake, John Terry aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwa kumpiga teke Alexis Sanchez.

  Lakini bao la kushitukiza la Ramires kabla ya mapumziko lilirejesha matumaini kwa Chelsea kabla ya Lionel Messi kukosa penalti na makosa ya safu ya ulinzi yakampa mwanya Fernando Torres kutimka kwa kasi kwenda kufunga bao lililokamilisha bei ya tiketi ya Chelsea kwenda Munich dakika ya mwisho mchezo.

  “Nini kiwango! Najua ngoma ilikwishakuwa ngumu wakati huo, lakini tulipigana hadi mwisho sana," alisema Lampard. “Najua watu walitaka kuona soka maridadi, lakini tukiwa 10 kwa dakika 50 zilizosalia na tukiwa nyuma kwa mabao mawili na kucheza namna ile- tulionyesha morali ya aina gani - ngumu kuamini tulivyoshughulika!

  “Saa zilikuwa kama zinakwenda taratibu sana kipindi cha pili, lakini nilikuwa na fikra utakuwa usiku wetu. Wote mnafahamu wanaweza kufunga wakati wowote kwa sababu ya wachezaji wao walionao kwenye timu, lakini kulikuwa kuna kujituma juu yetu.

  “Katika mchezo unaopata kile unachostahili na tulikuwa wote wamoja na tulipigana na matunda yake ni matokeo mazuri tuliyopata.”

  Lampard alisema hakuwa mwenye kujiamini kwamba mchezo huo ulikuwa salama hadi pale Torres alimpomzunguka Victor Valdes dakika ya mwisho na kuihakikishia Chelsea kutinga fainali dakika ya mwisho ambako watamenyana ama na Bayern Munich au Real Madrid mwezi ujao.

  “Niliweza kutulia wakati Fernando alipomzunguka kipa,” alisema Lampard. “Kipindi cha pili kilionekana kama kimechukua muda mrefu - hata zilipobaki sekunde, kilichotokea miaka michache iliyopita walipotufunga bao la ushindi dakika za mwishoni, bado ilikuwa akilini mwetu wote.

  “Unashangaa kama ingetokea tena na wakati huo, bahati ilikuwa upande wetu, lakini umeifanya bahati yako mwenyewe na tulistahili matokeo hayo.”

  Kiungo huyo alisema hakuona Terry akitolewa nje kwa kadi nyekundu, lakini anampa pole sana Nahodha, ambaye sasa ataikosa fainali.

  “Hapana, sikuona tukio hilo," alisema. "John alisema alimkimbilia kwa nyuma. kwa kweli sikuona hilo, lakini nachoweza kusema namfikiria yeye huko huko. Tulikuwa pamoja katika hili na tumeshinda usiku huu, pamoja. kama atakosa fainali na tutaendelea na tutashinda, ambayo ni ombi kubwa, kisha ataibuka na kuungana nasi huko.

  “Sitaki hata kufikia nani tutacheza naye kwenye fainali. Real na Bayern ni timu mbili nzuri sana sana, na siwezi kusema tunataka tukutane na nani – ni timu mbili babu kubwa. Ni kweli Chelsea wana heshima kubwa na upendo wa hali ya juu kwa Jose Mourinho baada ya kile alichokifanya hapa, lakini tuko sawa. Hakuna mtu aliyetarajia tungefuzu, hivyo ukweli ni tuko kwenye fainali ni jambo la kujivunia kwetu.”
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LAMPARD AWAPONGEZA WENZAKE, ASEMA YEYOTE AJE IWE REAL AU BAYERN WAKO TAYARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top