Fernando Torres amefunga hat-trick yake ya kwanza jioni tangu ajiunge na Chelsea na kuwaongezea matumaini The Blues kumaliza Ligi Kuu England ndani ya Nne Bora, baada ya kuifunga 6-1 QPR.
Daniel Sturridge alifunga dakika ya 45 kabla ya John Terry kufunga naye na Torres akafunga mawili na kufanya ushindi wa 4-0 baada ya dakika 25.
Torres alihitimisha hat-trick kipindi cha pili kabla ya Florent Malouda kufunga na kuwa 6-0 na Djibril Cisse akaifungia QPR bao la kufutia machozi. Chelsea sasa inapanda hadi nafasi ya tano, huku QPR ikiwa juu ya eneo la hatari ya kushuka daraja kwa tofauti ya mabao tu
.