• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 24, 2012

  SIMBA WAINGIA KAMBINI TAYARI KUUWA WASUDAN


  Wachezaji wa Simba SC

  WAWAKILISHI wa Tanzania, kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Simba wameingia kambini leo kujiandaa na mchezo wao kwanza wa hatua ya 16 Bora dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan, utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii.
  Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema leo kwamba timu imeingia kambini katikati ya Jiji, kujiandaa na mchezo huo wakiwa na  matumaini makubwa ya kushinda.
  Hata hivyo, Kaburu alisikitika kwamba wapinzani wao hawajatoa taarifa rasmi ya kuwasili kwao, ingawa wao wamekwishatuma taarifa za mchezo huo kwa chama cha soka Sudan.
  Alisema wachezaji wao wana morali ya hali ya juu na mchezo huo na benchi la ufundi limeahidi kushinda mabao mengi zaidi ili kujiweka katika mazingira mazuri katika mechi yao ya marudio.
  “Kikosi kipo vizuri na wachezaji wamepania kushinda mchezo huo, hata hivyo mchezaji Shomari Kapombe alipata maumivu ya mguu kidogo katika mchezo wa juzi dhidi ya Moro United  na anaendelea na matibabu kama akiwa vizuri kocha anaweza klumpanga hiyo jumapili,”aliongeza kaburu.
  Aidha, Kaburu alisema waamuzi wa mchezo huo  Nhleko Simanga Pritchard, Mbingo Petros Mzikayifani na Sibandze Thulani, Swaziland na Fakudze Mbongiseni Elliot, pamoja na Kamishna,  Kayijuga Gaspard wa Rwanda wanatarajiwa kuwasili Ijumaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA WAINGIA KAMBINI TAYARI KUUWA WASUDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top