• HABARI MPYA

  Saturday, April 28, 2012

  MAN UNITED YANASA KIUNGO MKALI BUNDESLIGA


  Shinji Kagawa - Dortmund v Bayern
  Getty Images
  EXCLUSIVE
  By Greg Stobart

  KLABU ya Manchester United inataka kumsajili nyota wa Borussia DortmundShinji Kagawa na taarifa zinasema mabingwa hao wa Ujerumani wamepoteza matumaini ya kumbakiza kiungo huyo mshambuliaji.
  Rais wa Dortmund, Dk Reinhold Rauball amesema kwamba anahofia Kagawa hatasaini kuongeza mkataba wakati United wameonyesha nia ya kumsajili kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa kumpa mshahara wa pauni 95,000 kwa wiki.

  bongostaz.blogspot.com inatambua kwamba Sir Alex Ferguson amekuwa akimmezea mate kwa muda mrefu mwanasoka huyo wa kimataifa wa Japan, ambaye thamani yake ni pauni Milioni 12 wakati mkataba wake unaisha msimu ujao.

  United inahaha kusaka kiungo mbunifu na imemnyooshea kidole Kagawa - ambaye amekuwa katika kiwango cha juu  msimu huu na amefunga mabao 16  - akiingia kwenye orodha ya wachezaji wengine kama Luka Modric na Eden Hazard wanaotakiwa na klabu hiyo.

  Vinara hao wa Ligi Kuu England pia wanataka kumsaini Kagawa pia kwa sababu za kibiashara na hiyo inafuatia manufaa waliyopata kwa kuwa naye mtu mwingine kutoka Mashariki ya Mbali, Ji-Sung Park.

  ATAJIUNGA NA TIMU YA USHINDI?


  Kagawa, ambaye pia amekuwa akiwatoa udenda Arsenal na Chelsea, inaaminika amepewa ofa ya pauni Milioni 2.4 kwa mwaka kurefusha mkataba wake kwa mwaka hadi 2016, pamoja na kuongezewa mshahara. Atakuwa anapata mara nne ya mshahara anaopata sasa akitua Old Trafford.

  Kagawa alitua Dortmund akitokea Cerezo Osaka mwaka 2010 na alifunga bao dhidi ya Gladbach wiki iliyopita wakati kikosi cha Jurgen Klopp kikijihakikishia taji la pili mfululizo la Bundesliga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YANASA KIUNGO MKALI BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top